Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako.
6 na 9 zinafanana,
kutegemea na upande uliosimama.

Mambo tunayoyapa umuhimu katika maisha, yanategemeana sana na tunachokiamini,…
Kuna vitabu ukisoma, kesho yake ukaulizwa ‘Hicho kitabu kinahusu nini?’, jibu lako linaweza likawa fupi sana, sentensi mbili.
Kuna kitabu ukikisoma, utataka kukirudia. Na sio hivyo tu, hata kama hujaulizwa, utakua tayari kukisimulia,
unaweza usiishie hapo, unaweza ukaamua kumnunulia kabisa! Utahisi kama anapoteza kama hatakisoma kama wewe ulivyokisoma.
Hivi vitabu utakavyoona, vitakuachia alama ya kutaka kusimulia, tukianza na;
1. The Richest Man in Babylon / Tajiri wa Babeli

Ni kitabu kilichoandikwa na mfanyabiashara, George S. Clason, na kilitoka mwaka 1926. Mpaka sasa kimetafsiriwa kwa lugha takribani 32.
Ni kitabu ambacho kinatumia hadithi za muda wa kale katika mji wa Babeli, kuonyesha kanuni za uchumi binafsi kama;
✔ kuweka akiba,
✔ kulipa madeni,
✔ kujiandaa na fursa,
✔ kuongeza kipato,
✔ kuwekeza, na
✔ kutokua na tamaa na pesa ya haraka.
‘dhahabu huja kwa wingi kwa yule ambaye huweka akiba moja ya kumi
ya kipato chake, na kuitumia akiba kuwekeza kwa ajili ya wakati ujao’
2. Rich Dad, Poor Dad / Baba Tajiri, Baba Maskini

Ni kitabu kilichoandikwa na mfanyabiashara, Robert Kiyosaki, na kilitoka mwaka 1997. Mpaka sasa kimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 50.
Ni kitabu ambacho kinatumia hadithi ya Robert ambaye alikuwa na baba wawili.
Baba wake wa kumzaa, ndio maskini na baba wa rafiki yake, ndio tajiri.
Sio kwamba baba yake hakuwa na hela. Baba yake alikua ni msomi na aliyeajiriwa ila hakuwa na mtazamo kuhusu kujenga utajiri wa kudumu…
ambao haukutokana na mshahara bali kimeonyesha umuhimu wa,
✔ kujenga na kukusanya mali ‘assets’,
✔ kuwa na elimu ya fedha ambayo haifundishwi mashuleni,
✔ kujenga biashara,
✔ kufanya uwekezaji,
✔ kuwa na mapato tulivu ‘passive income’, na
✔ kuwa na mtazamo chanya wa kifedha ‘positive mindset’.
3. The Psychology of Money

Ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi, Morgan Housley, na kilitoka mwaka 2020.
Ni kitabu kinachohusu mtazamo na saikolojia ya utajiri, tamaa, na furaha. Kinaonyesha mambo muhimu kama;
✔ mafanikio ya kifedha inahusisha sana tabia kuliko akili,
✔ tofauti ya kuwa tajiri na kubaki na utajiri,
✔ vitu ghali vinaonyesha matumizi na sio utajiri,
✔ utajiri sio lazima kwamba mtu hakosei au alikosea kidogo,
✔ kujipa nafasi ya kukosea, na
✔ kuheshimu nguvu ya muda katika kuwekeza.
4. Maamuzi Juu ya Fedha Inayopita Mkononi Mwako Yaweza Kukufanya Uwe Tajiri au Maskini

Ni kitabu kilichoandikwa na mhubiri, Christopher Mwakasege, na kilitoka mwaka 2016.
Ni kitabu kinachohusu jinsi ya kufanya maamuzi sahihi ya kila fedha unayoipata. Fedha ambayo unaipata ndio itakufanya kuwa tajiri au maskini.
Kitabu kinaonyesha umuhimu wa;
✔ kuweka akiba,
✔ kutotumia kiasi kikubwa kuliko unachokipata,
✔ kutengeneza vyanzo vingi vya mapato,
✔ kuwekeza,
✔ kutodharau pesa ‘kidogo’ na
✔ kuepuka makosa ya kifedha.
5. Kustaafu

Ni kitabu kilichoandikwa na mwekezaji, Emilian Busara, kinachohusu kujiandaa kuhusu kustaafu, hasa kwa waajiriwa.
Lakini, mwandishi amesisitiza kwamba kustaafu sio kwa ajili ya wazee peke yake…
bali kila mtu anapoanza ajira anatakiwa ajue kwamba safari hiyo ina mwisho wake.
Mambo mengine muhimu ni kama;
✔ umuhimu wa kuwa na afya nzuri,
✔ kujenga mapato yanayodumu,
✔ matumizi ya pensheni,
✔ mambo ya kujishughulisha nayo baada ya kustaafu,
✔ kustaafu kwa malengo na
✔ kutunza mahusiano na jamii.
Ili usogee hatua nyingine kuhusu pesa yako, unaweza ukajifanyia tathmini ya uchumi binafsi kwa kujibu maswali machache, kama inavyoonekana hapa chini;

Utatumiwa majibu yako kwenye email ili ugundue wapi pa kuanza kuboresha.
Lakini pia, kama ungependa kujua namna ya kuanza na uchumi wako binafsi, unaweza ukasoma hapa.
Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na unaweza ukatuandikia kupitia Whatsapp.
PS:
6 na 9 zinafanana, kutegemea na upande uliosimama.
Kuwa na mtazamo wa chanya ‘positive mindset’ kuhusu fedha kutakusaidia kufanya maamuzi yatakayokusaidia.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
References:
1] The Richest Man in Babylon, George S. Clason
2] Rich Dad Poor Dad, Robert Kiyosaki
3] The Psychology of Money, Morgan Housley
4] Maamuzi Juu ya Fedha, Christopher Mwakasege
5] Kustaafu, Emilian Busara
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
