Huna haja ya kununua hisa ya bei kubwa ili upate faida kubwa. Pitia sababu hizi 5 kwa manufaa yako.
Umesikia kuhusu uwekezaji kwenye hisa,
Na unajua kwamba hisa ni umiliki wa sehemu ya kampuni au biashara…
Na hisa zina bei tofauti kulingana na makampuni husika.
Ila, hujajua bei ya hisa inahusiana vipi na faida utakayoipata.
Kama uko kwenye hali hii, ujumbe huu ni kwa ajili yako.
Lakini kabla hatujaendelea, inawezekana ungependa kupitia tena utangulizi wa hisa.
Mnamo tarehe 4 Julai 2025,
makampuni yaliyopo kwenye Soko la Hisa (DSE: Dar-es-Salaam Stock Exchange) ambayo yaliuza na kununua hisa kwa siku hio,
…bei za hisa zilianzia shilingi 145/= (DCB Commercial Bank) mpaka shilingi 16,010/= (TCC: Tanzania Cigarette Company – Sigara) kwa hisa moja.
Faida kuu mbili za kuwekeza kwenye hisa kama unavyojua, ni kukuza mtaji ‘capital gain’ na kutoa gawio ‘dividend income’.
Fedha yako inakua kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa na Gawio unapata kutoka kwenye faida ya kampuni kwenye mwaka huo wa fedha.
Sasa tukirudi kwenye mada yetu kuu, tuone…
Jinsi gani bei ya hisa ya kampuni fulani haihusiani moja kwa moja na faida utakayoipata;
1. Bei ya Hisa Haionyeshi Moja kwa Moja Faida ya Baadaye
Faida utakayoipata ukiwekeza kwenye hisa, ikiwa ni gawio na/au kukua kwa mtaji inategemea sana na,
Uwezo wa kampuni kutumia mtaji wake kutengeneza faida, pia
Na faida ya kampuni hio kabla ya makato ya riba na kodi.
Kwahio, hisa inaweza ikawa na bei ndogo au bei kubwa lakini kama haitengenezi faida endelevu,…
wewe mwekezaji hautapata faida endelevu pia.
2. Uchambuzi Utakaofanya Kabla ya Uwekezaji Utakupa Uhalisia
Sambamba na kupata elimu ya awali ya hisa, itakubidi kuchambua makampuni kulingana na,
✔ Ubora wa Kampuni (Qualitative Analysis)
✔ Historia ya Mapato, Faida, Madeni, nk. (Qualitative Analysis)
Hivyo, bei ya hisa inaweza ikawa na bei ndogo au bei kubwa lakini kama haina uongozi mzuri,…
au kama kiwango chake cha madeni kimezidi mapato kwa asilimia kubwa,..
…uwezekano wa kupata gawio au kukua kwa bei ya hisa unapungua.
3. Bei ya Hisa Inaweza Kuwa Ghali Kuliko Thamani Halisi ya Kitabu
Kila kampuni ina thamani ya kitabu (Book Value) ambayo ni jumla ya mali zake ukitoa madeni yake yote.
Hii inakua thamani halisi ya kampuni.
Mabadiliko ya bei ya hisa yanaweza yakapelekea hisa kuwa;
✔ chini ya thamani halisi ‘underpriced’,
✔ thamani ya wastani ‘fairly priced’, au
✔ thamani ya juu ‘over priced’,
kwa muda huo.
Kwahio, bei ya hisa inaweza ikaonekana sio kubwa lakini ni ghali ukilinganisha na thamani halisi ya kampuni.
4. Kampuni Inaweza Isitoe Gawio Hata Kama Imepata Faida
Kila kampuni ina sera yake ya gawio.
‘Kampuni A itatoa asilimia A ya faida yake kama gawio kwa wawekezaji.’
Lakini, usisahau kwamba gawio inatokana na faida. Kwahio, kampuni inaweza ikaamua kurudisha faida ya mwaka huo kwenye biashara hio,…
…kwa ajili ya kukuza kampuni.
5. Bei ya Hisa Inaweza Isibadilike kwa Muda Mrefu
Bei ya hisa inakua kutokana na matarajio chanya ya wawekezaji (demand and supply).
Kadri ‘demand’ inapokua kubwa, bei ya hisa inaongezeka.
Lakini, inaweza ikafika muda bei ikaacha kubadilika, kwasababu ya;
✔ ‘Demand’ imepungua ya hisa husika, au
✔ Kampuni imeshakua kubwa na inatoa faida yake kama gawio.
Na kama bei ya hisa haiongezeki, basi unakosa faida ya kukuza mtaji ‘capital gain’.
Hapa chini, unaweza kupakua (download) tracker ya kufuatilia uwekezaji wako wa Hisa, hata kama bado haujaanza kuwekeza:

Na kama ungependelea uwekezaji wa namna nyingine, unaweza kupitia Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji na Uwekezaji katika Hatifungani (Bonds).
Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Kiwango cha chini cha kununua ni hisa 10 tu! Hauhitaji mamilioni kuanza.
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
References:
1] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz
2] Dar-es-Salaam Stock Exchange Market Report, Friday, 4th July 2025
3] The Little Book That Still Beats the Market, Joel GreenBlatt
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
