Mbinu 7 ULIZOWAHI KUSIKIA Kuhusu Bajeti, Akiba, na Matumizi Hata Ukiwa na KIPATO KIDOGO

Jifunze jinsi ya kuweka bajeti, kuepuka madeni, kuweka akiba, na kufuatilia matumizi hata ukiwa na kipato kidogo.

Kukosa nidhamu ya fedha haihusiani na ukubwa wa kipato. 

Changamoto kama kutokuwa na bajeti, kutoweka akiba, kutokumudu matumizi, hata kusongwa na madeni zinawakuta…

…wenye vipato vikubwa, wastani na vipato vidogo.

Unadhani ni kwanini?

Ni kwasababu, nidhamu ya fedha ni tabia. Na wewe ndiye unayeijenga tabia, kama utaridhia.

Ripoti ya Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Huduma za Kifedha nchini, FinScope Tanzania ya 2023, imeonyesha kwamba…

asilimia 66% ya watanzania wanapata changamoto kumudu gharama za kawaida za maisha.

Lakini pia, 


akiba ni kipaumbele baada ya mapato kwa watu asilimia 4% tu huku matumizi

(ukitoa chakula na mavazi) kuzidi kwa asilimia 77%.

Sasa, bila kupoteza muda, tukianza na mbinu za…

Kuwa na bajeti,

1. Ujue kutofautisha kati ya matumizi ya lazima ‘needs’ na yasiyo ya ulazima ‘wants’

Mara nyingi matumizi yasiyo na ulazima yana gharama zaidi kuliko matumizi ya msingi, na

…utapata msukumo zaidi kutumia pesa kwenye ‘wants’ kuliko kwenye ‘needs’.


Anza na matumizi yako ya msingi kama chakula, usafiri, na malazi.

2. Fuatilia matumizi yako yakoje, kila shilingi, angalau mara 1 kwa wiki.

Bajeti ya namna hii inaitwa ‘Zero-Based Budgeting’.

Ukifuatilia matumizi yako kwa angalau mwezi mmoja, utajua kirahisi udhaifu wako uko wapi.

Mfano;

Kama kipato chako ni 600,000/= kwa mwezi, baada ya mwezi kuisha utajua wapi unatumia hela zaidi,

…wapi wa kupunguza, wapi pa kuboresha au kurekebisha. Namba zitakupa majibu.

3. Weka akiba KABLA ya kufanya matumizi na sio kuweka akiba kwenye pesa iliyobaki.

Kwenye kuweka akiba,

Mfano;

Kama kipato chako ni 600,000/= kwa mwezi, tenga pembeni angalau asilimia 10% yani 60,000/= ndipo uanze kuipangia 540,000/=.

Itakua ngumu kwako kuweka akiba toshelevu ukishaanza kuitumia pesa mara tu unapoipokea.

4. Epuka kutumia pesa ili kuonekana na watu wengine au kwasababu ya matumizi unayoyaona kwa watu wengine.

Katika kumudu matumizi,

Kama wenzako wanaenda maeneo ya starehe ambayo huwezi kumudu kwa muda huo, usione aibu kulikubali hilo…

kwasababu hio ndio ‘urefu wa kamba yako kwa sasa’.

Wengine wakitoa michango ya sherehe ya 50,000/=, haina ubaya wowote kama wewe ukatoa unachokimudu.


Utakapotumia ili kuonekana, utapata stress ya pesa na watu wala hawatakuona.

5. Usitumie zaidi ya asilimia 30% ya kipato chako kwa ajili ya malazi ‘housing’

Jumla ya gharama za malazi kama kodi, umeme, maji, usafi na ulinzi zikiwa juu kulingana na kipato chako,

…utahangaika na matumizi mengine.

Kwa mfano;

Kama ni 600,000/= unaipata, halafu ukatumia zaidi ya 180,000/= kwa ajili ya nyumba kwa mwezi, inaweza ikawa ngumu…

kukitunaisha hicho kipato na mwezi unaofuata.

6. Usiache kutafuta fursa za kuongeza kipato na kuwa na malengo ya kifedha.

Kwa maana nyingine, usijikatie tamaa na ukaukubali umaskini. Uchukie umaskini.

Kuonewa huruma na kulalamika hakujawahi kumkomboa mtu, zaidi sana unaweza ukapata magonjwa kwasababu ya msongo wa mawazo.

Ni watu wengi wamezaliwa katika hali duni lakini hawajafa katika hali duni. Jione kama mmoja wao.

Kuna quote nzuri sana inasema,

You are born looking like your parents, You die looking like your decisions

Inamaanisha, unapozaliwa unafanana na wazazi wako ila unapokufa unafanana na maamuzi yako.

Kwahio, usikate tamaa mpaka unapotimiza unachokitamani.

Hakuna mtu wa kukufanyia hilo isipokuwa wewe.

7. Epuka madeni kwa kupunguza matumizi yasiyo ya msingi na kuweka akiba itakayoweza kukusaidia changamoto za ghafla zinapotokea.

Asilimia kubwa inayochukuliwa na watu ni kwa ajili ya matumizi binafsi, mbali na kuwekeza kuzalisha kwenye shughuli za uchumi.

Tunakopa kwa ajili ya,

✔ kuvaa vizuri, 

✔ kubadilisha furniture za ndani, 

✔ kutembelea gari kali, 

✔ kusafiri kwa ajili ya utalii, 

✔ kumudu gharama za misiba, 

✔ kuchangia sherehe,

✔ kulipa ada,

✔ kuhudumia ndugu na marafiki wasio na nidhamu ya pesa zao,

…lakini katika yote hapo juu, hakuna kinachozalisha pesa.

Zaidi ya kukuzalishia magonjwa na msongo wa mawazo.

Hakuna kibaya kati ya hivyo vyote…

lakini basi tafuta jinsi ya kuongeza kipato huku ukivifanya kwa kiasi.

Kama ungependa kujifanyia tathmini ya uchumi binafsi kwa kujibu maswali machache, kama inavyoonekana hapa chini;

Utatumiwa majibu yako kwenye email ili ugundue wapi pa kuanza kuboresha.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.

PS: 

Umezaliwa ukifanana na wazazi wako, lakini utakufa ukifanana na….(utamalizia) :)

Haujachelewa kuanza!

Kila la kheri.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

References:

1] FinScope Tanzania 2023 Key Findings Launch, 10th July 2023, Bank of Tanzania Auditorium

2] FinScope Tanzania 2023

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

Share your love
Grace Sambali
Grace Sambali
Articles: 55