Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani
Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya mtandao lakini…
Wewe ni muislamu na ungependa kuweka akiba na kuwekeza mahala ambapo panaendana na misingi yako ya imani.
Kuna wadau katika Soko la Fedha waliolifikiria hili, na walio kufikiria wewe.
Rasilimali za Fedha za Kiislamu (Islamic Financial Products) zinakua zimezingatia;
✔ Kanuni za Shariah katika uwekezaji na miamala inayofanyika,
✔ Mgawanyo wa Hatari ya Kupoteza ‘Risk’ kati ya mkopaji
Na…
✔ Upatikanaji wa Huduma za Kifedha kwa wale ambao kwao, huduma za kibenki za kawaida haziendani na msingi wa kidini.
Rasilimali za Kuweka Akiba (Islamic Saving Products) kwa ajili yako ni;
✔ Islamic Savings Account
Hii hazitofautiani na akaunti ya benki ya kawaida ila inakua na kanuni ya kukupatia sehemu ya faida na sio riba.
✔ Akaunti ya Mudarabah (Mudarabah Account)
Upande mmoja unatoa mtaji na upande mwengine (wewe) unatoa ujuzi halafu faida inagawanywa kwa makubaliano (predetermined ratios).
Na,
✔ Akaunti ya Wadi’ah (Wadi’ah Account)
Hii akaunti inakua inalinda mtaji wako kuliko kupata faida.
Rasilimali za Uwekezaji (Islamic Investment Products) kwa ajili yako ni;
✔ Sukuk (Islamic Bonds)
Unapata mapato ya Hatifungani, yaani malipo ya kuponi yanatokana na faida inayopatikana na sio riba.
Mfano mzuri ni Sukuk Bond ya KCB Bank na Sukuk Bond mbili (2) za Serikali ya Zanzibar (kwa Shilingi TZS na kwa Dollars $$)
✔ Mudarabah (Profit Sharing)
Upande mmoja unatoa mtaji na upande mwengine (wewe) unatoa ujuzi halafu faida inagawanywa kwa makubaliano (predetermined ratios).
✔ Musharakah (Joint Venture)
Mara nyingi hutumika katika miradi ya ujenzi.
Watu au taasisi tofauti zinachangia mtaji wa mradi halafu wanagawana faida au hasara kutokana na namna walivyochangia.
✔ Murabaha (Cost-Plus Financing)
Benki inanunua rasilimali (an asset) kwa ajili yako na inauza kwa bei ya kupata faida. Halafu wewe, unalipa kwa awamu, pamoja na faida yake.
✔ Ijara (Lease Financing)
Unakopeshwa rasilimali na utalipa kwa mfumo wa kodi. Halafu umiliki utakua ni wako pale muda wa hiyo kodi hio utakapoisha.
Je, rasilimali hizi ni kwa ajili ya waislamu peke yake?
Hapana…
Ila ni lazima uzingatie taratibu zote zinazohusiana na huduma hio.
Tembelea tawi la benki unayoitumia ili kufahamu ni huduma gani za akiba na uwekezaji walizonazo, au…
Benki zinazo zingatia misingi ya Kiislamu kama hizo kama AMANA Bank na CRDB Al Baraka.
Je, ni mfuko wa pamoja wa uwekezaji unaotafuta kuanza nao?
Kuna Alpha Halal Fund ulioanzishwa na Alpha Capital Limited na,
mfuko wa iImaan ulioanzishwa na iTrust Finance Limited.
Kama umeshaanza uwekezaji au kuweka akiba kwa mfumo wa ‘liquid assets’…
Tumia tracker kama ilivyoonyeshwa hapa chini kwa urahisi wa kufuatilia uwekezaji wako kila mwezi.

Fuatilia Instagram kwa ajili ya free content, bonyeza button hapo chini kwa mawasiliano ya Whatsapp.
PS:
Bado una nafasi ya kushiriki kwenye Soko la Fedha, kuweka akiba na kuwekeza kwa ujasiri.
Anza leo!
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
References:
1] CRDB AlBarakah Banking,https://crdbbank.co.tz/en/for-you/al-barakah-banking
2] AMANA Bank | Islamic Bank in Tanzania, https://www.amanabank.co.tz/
3] Financial Educator Certification, Covenant Institute of Tanzania and Bank of Tanzania (BOT)
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
