Hauhitaji mamilioni ili kuanza kuwekeza. Jua jinsi ya kuwekeza kwa kianzio cha TZS 10,000/= tu.
Umetamani kuwekeza lakini ukadhani unahitaji kiasi kikubwa sana kuanza?
Kama jibu lako ni ndio, fuatana nami mpaka mwisho wa ujumbe huu.
Emmanuel, kijana wa miaka 26 alikuwa na tabia ya kuweka akiba. Aliweka akiba yake benki, na kiasi kingine nyumbani.
Lakini, kila alipokusanya pesa ya kutosha aliishia kuitumia, kwasababu alijua ‘nyumbani hela ipo’…
…baada ya kuitumia, ilibidi aanze mapambano upya.
Ile iliyokuwepo benki ilikua inapungua pia. Zilikua ni zile gharama za mwezi za akaunti, mara makato ya kutoa pesa kwenye ATM,…
…akaamua kutafuta njia mbadala.
Ndipo akasikia kuhusu mifuko ya pamoja ya uwekezaji, akaamua kuulizia zaidi akagundua kwamba…
✔ aliweza kuanza na kiasi kidogo,
✔ hela yake ilikua na uwezekano wa kukua badala ya kupungua tu,
✔ angeweza kuitoa pesa yake bila makato au kwa makato madogo sana, na
✔ angeweza kuanza muda wowote anaohitaji.
Hakupoteza muda, akafungua akaunti yake ya kwanza kwenye mfuko wa pamoja wa uwekezaji.
Kabla hatujaendelea,…
Ujue ya kwamba akiba ni kutenga fedha na kuikusanya, lakini Uwekezaji ni kuifanya fedha ulioikusanya izalishe fedha zaidi.
Hivyo basi,
Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji ni mfuko ambao watu wengi huwekeza pesa zao na huwa unasimamiwa na wataalamu wa fedha.
Baada ya taasisi husika kukusanya fedha hizo,…
…wao pia wanawekeza katika Soko la Fedha ili kuzalisha faida ambayo baadae hugawanywa kwa wawekezaji.
Mifuko ya namna hii huwa inaahidi ongezeko la pesa yako mpaka asilimia 12% kwa mwaka…
ingawa hautakiwi kusahau ya kwamba kila uwekezaji una hatari / ‘risk’ ya kupoteza pesa.
Hivyo, kwa kiasi kikubwa unaweza ukategemea hela yako kuongezeka badala ya kupungua.
Kwetu Tanzania kuna mifuko zaidi ya 15 ya pamoja, baadhi ikiwemo;
✔ Mfuko ya Umoja (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Watoto (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Bond (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Ukwasi (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Faida
✔ M-Wekeza, na
✔ Mfuko wa Sanlam Pesa
Ukiachana na faida kama kianzio kidogo, pesa yako kukua, usimamizi wa wataalamu, na kuwepo mifuko mingi utakayoweza kuchagua kutokana na malengo yako…
Lakini pia,
- Utaweza ukajiunga kupitia simu muda wowote na baadae kujaza fomu katika taasisi husika kwa urahisi,
- Utaweza kupata pesa yako hapo hapo hadi ndani ya siku 3 za kazi kulingana na mfuko uliouchagua,
- Itakusaidia kukusanya hela yako ya malengo yako ya muda mrefu,
- Bila kuacha, kutenga akiba kwa ajili ya malengo yako mengine.
Mifuko mingi imeweka namna ya kuangalia fedha uliowekeza kupitia simu yako ya mkononi muda wowote unaotaka.
Kama ungependa kujua namna ya kuchagua mfuko utakaoendana na malengo yako, unaweza ukasoma hapa…
na utapata urahisi wa kufuatilia uwekezaji wako kila mwezi kama utapakua (download) tracker hapa chini:

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
Hatujamalizana!
Kama una malengo ya kufikia kiwango fulani cha fedha ndani ya miaka kadhaa, unaweza ukafahamu utakachotakiwa kuweka kila mwezi,
…kupitia: UTT Monthly Investment Plan
Anza maisha yako ya uwekezaji kwa shilingi 10,000/= tu. Usiidharau pesa ‘kidogo’.
PS:
Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza.
Anza leo!
Wako katika pesa,
Gracing Money!
Marejeo:
1] UTT AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan
2] UTT-AMIS, uttamis.co.tz
3] Watumishi Housing Investment, whi.go.tz
4] M-Wekeza, vodacom.co.tz
5] Sanlam Pesa Money Market Fund, invest-tz.sanlameastafrica.com
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
