Soma hii kabla haujachagua mfuko wa uwekezaji unaoendana na malengo yako ya kifedha.
Umesikia mifuko mingi ya pamoja ya uwekezaji na hujui uchague upi?
Kama jibu lako ni ndio,
…mpaka mwisho wa ujumbe huu, utakuwa umeshapata majibu unayotafuta.
Lakini, anzia hapa kama haujafahamu kuhusu mifuko ya uwekezaji.
Kuna zaidi ya mifuko 15 ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini kwetu,…
baadhi ikiwa;
✔ Mfuko ya Umoja (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Watoto (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Bond (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Ukwasi (UTT Amis)
✔ Mfuko wa Faida
✔ M-Wekeza, na
✔ Mfuko wa Sanlam Pesa.
Kila mfuko una malengo yake na faida yake ya kuutofautisha, lakini swali ni je, malengo yako ni yapi?
Hili ndo swali moja rahisi ambalo kama utaweza kulijibu, maswali yako yote mengine utayajibu kwa haraka sana.
Tuanze na;
1. Aina ya Mapato ya Mfuko Husika
Faida mbili (2) kuu za mifuko ya pamoja ni Kukuza Mtaji na Kupata Gawio.
Kama haya ndo malengo makuu mawili, inamaana mfuko unaouchunguza ni kwa ajili ya sababu moja wapo;..
…kwamba lengo kubwa la mfuko huo ni kukuza mtaji au kutoa gawio.
Kutumia mifano saba ya mifuko kwenye ukurasa wa kwanza, Mifuko ya Watoto na Umoja inakuza mtaji na Mfuko wa Bond unatoa gawio,
…lakini pia,
2. Faida Maalum ya Mfuko Huo
Mfuko unaweza ukawa unakuza mtaji au unatoa gawio lakini unaweza ukawa na faida maalumu ambayo wewe hauhitaji.
Mfano;
Mfuko wa Watoto ni maalumu kwa watoto. Kwahio unaweza ukataka kukuza mtaji lakini sio kwa ajili ya mtoto.
Mfuko wa UTT wa Wekeza Maisha unakuza mtaji lakini huwezi ukatoa mpaka baada ya miaka mitano. Huu unawafaa zaidi wanaojiandaa kustaafu.
Mfuko wa Bond unatoa gawio kila mwezi na kila nusu mwaka, lakini wewe unaweza ukawa unahitaji gawio kila robo mwaka,
…kwahio itakubidi kuchagua mfuko mwengine.
Kingine ni,
3. Kianzio cha Kuwekeza Kwenye Mifuko
Ni muhimu kufahamu kiwango cha chini cha uwekezaji cha mfuko husika.
Kianzio cha mifuko mingi kama mifuko ya Umoja, Watoto, Faida, M-Wekeza ni 10,000/= na mingine 50,000/= (kama Mfuko wa Bond),…
100,000/= (for Liquid and iCash Funds), all depending on the type of income it provides, whether it is an income or capital growth.
4. Muda wa Uwekezaji
Unaweza ukachagua mfuko unaoendana na muda unaotaka kuwekeza, kama ni muda mfupi au muda mrefu.
Muda wa Kizuizi:
Mifuko kama Faida, Watoto na Wekeza Maisha inaweza ikachukua miezi mitatu mpaka miaka mitano ya kizuizi kwenye kutoa fedha.
Na kabla ya kuchagua mfuko ujue kama ni kweli hautahitaji kutoa pesa katika kipindi chote cha kizuizi.
Na la mwisho ni,
5. Urahisi wa Kutoa Fedha
Ukiachana na muda wa kizuizi,
Unatakiwa kujua kwamba unahitaji kutoa hela yako ndani ya muda mfupi,…
je, muda mfupi kwako ni siku ngapi?
Mfuko gani utakufaa utakapopata dharura?
Mifuko inatofautiana, kuanzia siku 3 hadi siku 10 za kazi (kama Mfuko wa Ukwasi, Umoja, na Timiza) au mfuko ambao unaweza kutoa hela hapo hapo…
kama M-Wekeza (ya Vodacom na Sanlam Investments).
Kwa, M-Wekeza, unaweza ukatoa pesa kupitia M-Pesa.
Tumia tracker kama ilivyoonyeshwa hapa chini kwa urahisi wa kufuatilia uwekezaji wako kila mwezi.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza.
Anza leo!
Wako katika pesa,
Gracing Money!
Marejeo:
1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz
2] Watumishi Housing Investment, whi.go.tz
3] M-Wekeza, vodacom.co.tz
4] Sanlam Pesa Money Market Fund, invest-tz.sanlameastafrica.com
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
