Hii ni AKIBA 1 Ambayo Hautakiwi Kuikosa, KWAKO na Kwenye Biashara YAKO!

akiba, haiozi!

Je, umeshawahi kusikia kwamba ‘Siwezi kuweka akiba, hela yangu ni kidogo’?

Au labda unafikiri kwamba biashara inatakiwa kujiendesha yenyewe, hakuna haja ya kuwa na akiba.

Ingekuwa vizuri sana kama kabla ya changamoto yoyote kukutokea wewe au kwenye biashara yako, ingekupa taarifa…

Lakini, haitokei hivyo.

Hii akiba moja pia inaweza kukusaidia kupunguza au kuepuka kabisa ulazima wa kuingia kwenye madeni yenye riba kubwa,

…kwa sababu tu haujajiandaa.

Ripoti ya Uchumi ya mwezi Juni 2025 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kwamba mikopo binafsi ndio inayoongoza,

katika taasisi zote za fedha, katika mwezi Mei 2025, kwa asilimia 35.7% ikifuatiwa na biashara (trade) asilimia 13.7%…

Kama hali ni hii, unaweza ukaamua kuwa na akiba ambayo itafanya changamoto zikukute ukiwa umejiandaa,

…na amani ya moyo isitoweke ndani ya muda mfupi.

Na akiba hii ni Mfuko wa Dharura. Ni kiasi unachokusanya kwa ajili ya kukabiliana na yale usiyoyategemea.

Ukiwa na Mfuko wa Dharura:

✔ Kuisimamia Pesa Yako.

Unapata muda wa kutafuta kazi nyingine au kuanzisha biashara bila stress pale ambapo kipato kinaposhuka au kinapokata 

Inaondoa ulazima wa kuingia kwenye madeni, hasa yenye riba kubwa unapopata gharama za ghafla kwako na katika biashara yako

✔ Inakusaidia kuwa na amani unapokutana na changamoto kama ugonjwa au matengenezo ya gari

✔ Utaweza kuendeleza utaratibu wako wa kuweka akiba bila ulazima wa kukatisha

✔ Inakuwezesha kufanya maamuzi ndani ya muda mfupi kwenye dharura kama safari za lazima, misiba na changamoto za kifamilia…

…na kwenye biashara, pale panapokua na marekebisho ya nyenzo au vifaa vya kuendeshea biashara,

pia maamuzi ya haraka fursa zinapotokea.

✔ Inasaidia kutosumbua uwekezaji wako wa muda mrefu kwa sababu ya kutoa hela kwa ajili ya dharura

Utaweza kulipa bili za watoa huduma na kodi pale malipo ya huduma yako yanapochelewa

Kutopoteza heshima ya jina la biashara yako katika kutimiza ahadi ya huduma unayoitoa kwa wateja wako

✔ Kutunza heshima ya biashara yako kwa kuwalipa uliowaajiri kwa wakati, sawa sawa na mategemeo yao

Jinsi ya Kujua Kiasi cha Mfuko wa Dharura Kulingana na Matumizi Yako

Cha kwanza, inabidi kufahamu wastani wa matumizi yako kwa mwezi kisha uzidishe kwa miezi ambayo ungetaka kuilinda amani yako…

Miezi mitatu (3) mpaka 6.

Kama ni biashara, utatumia gharama kubwa zaidi uliotumia kuendesha biashara yako kuliko miezi mingine, kisha uzidishe mara 3 mpaka 6.

Unaweza ukajua hesabu yako sasahivi, kwa kutumia Emergency Fund Planner.

Kama ulikua haujawahi kuwa na malengo ya kifedha, umeshapata kiasi cha kuanzia kuweka akiba.

Unaweza pia ukatumia Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji kuweka akiba.

Pale utakapofanikiwa kukusanya kiasi kubwa, changamoto unayoweza ukaitegemea ni kutaka kutumia pesa kwa matumizi yasiyo ya lazima…

Ukipata msukumo huo, bila kusahau malengo yako, unaweza ukailinda pesa yako kwa kuiwekeza sehemu ambayo hautaweza kuitoa kirahisi sana


…kama Hisa na Bondi.

Kama ungependa kufuatilia matumizi yako binafsi ya kila mwezi, pakua (download) tracker, kama inavyoonekana hapa chini;

au ukatumia apps za simu kama Moneylover, ambazo ni bure na rahisi kutumia, online na offline.

…na pia, unaweza ukafahamu zaidi kuhusu Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji, Hisa na Bondi ndani ya dakika chache zijazo.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na unaweza kuwasiliana nasi kwa Whatsapp na tutakurudia kwa wakati.

PS:

Kila 1,000,000/= ina shilingi 1,000/=, 2,000/=, na 5,000/= ndani yake. Usiidharau pesa ‘ndogo’.

Mfuko wa Dharura ni akiba ambayo hautakiwi kuikosa!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] Bank of Tanzania, Monthly Economic Review, June 2025.

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

Share your love
Grace Sambali
Grace Sambali
Articles: 55