Haujui Wapi Pa Kuwekeza? Hizi Ni TOFAUTI 12 RAHISI Kati ya BONDI, HISA, NA MIFUKO YA PAMOJA Kwa Mwekezaji Anayeanza!

Gundua tofauti kati ya bondi, hisa, na mifuko ya pamoja kwa uharaka na urahisi ili uanze kuwekeza leo.

Umesikia kuhusu uwekezaji, au

Umesikia watu wakiongelea bondi, hisa, na mifuko ya pamoja,…

lakini haujajua tofauti zao na wapi pa kuanzia kuwekeza.

Kama huyu ni wewe, katika ujumbe huu utagundua tofauti 12 muhimu, na utaweza kuchagua kwa urahisi wapi pa kuanzia.

Tukianza na kuwekeza,…


Ni kutumia fedha uliyokusanya au kuweka akiba ili kuzalisha fedha nyingine au faida.

Haya sasa, swali la kwanza la msingi;

Hisa, Bondi, na Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji ni nini?

Hisa ni umiliki wa sehemu ya kampuni au biashara. Kwa kiingereza inajulikana kama stock.

Hisa huuzwa kwa idadi na kwa bei ya kampuni husika yaani, stock price.

Mfano wa makampuni ya kitanzania yanayouza hisa ni Benki ya CRDB, Benki ya NMB, na Tanzania Portland Cement (Twiga Cement -TPCC).

Bondi ni uwekezaji ambao unaikopesha serikali au taasisi ili upate riba katika kipindi cha muda fulani.

Serikali, taasisi au kampuni inazitumia fedha hizo ili kuzalisha faida, na mwekezaji hurejesha anarudishiwa pesa yake baada ya muda wa bondi hio kuisha.

Bondi zinazotolewa na serikali zinaratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ‘Treasury Bonds’, na kuna bondi za;

✔ Manispaa ‘Municipal Bonds’, 

✔ Makampuni ‘Corporate Bonds’, na za

✔ Kimataifa ‘International Bonds’.

Mfuko ya Pamoja ya Uwekezaji ni mfuko ambao watu wengi huwekeza pesa zao na huwa unasimamiwa na wataalamu wa fedha.

Baada ya taasisi husika kukusanya fedha hizo, wanawekeza katika Soko la Fedha ili kuzalisha faida ambayo baadae hugawanywa kwa wawekezaji.

Mifuko ya namna hii huwa inaahidi ongezeko la pesa yako mpaka asilimia 12% kwa mwaka

ingawa hautakiwi kusahau ya kwamba kila uwekezaji una hatari / ‘risk’ ya kupoteza pesa.

Mfano wa mifuko hii ni kama,

✔ Mfuko ya Umoja (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Watoto (UTT Amis) 

✔ Mfuko wa Bond (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Ukwasi (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Faida

✔ M-Wekeza, na

✔ Mfuko wa Sanlam Pesa

Tofauti kati ya Hisa, Bondi, na Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji

HISABONDIMIFUKO YA PAMOJA
MAANAUmiliki wa sehemu ya KampuniKuikopesha serikali au taasisiWawekezaji wengi kwenye mfuko mmoja
ZINAUZWA KAMA (UNITS)…Hisa Moja, kulingana na kampuniBondi Moja, shilingi 100/=Kipande Kimoja (Net Asset Value per Unit)
FAIDAGawio (Dividend)Kukuza Mtaji (Capital Growth)Riba (Interest)Kukuza Mtaji; inategemea na bei utakayonunulia au kuuza1. Gawio (Dividend)2. Kukuza Mtaji (Capital Growth))
KIWANGO CHA FAIDAKiwango kinategemea na maendeleo ya kampuni ulilochagua  Kuanzia 8.5% kwa bondi za miaka mitatu na kuendeleaAhadi ya mpaka 12% kwa mwaka
KIWANGO CHA CHINI CHA KUANZIABei ya Hisa 10 ya kampuni utakalochaguaKuanzia 500,000/= mpaka 1,000,000/= (inategemea aina ya bondi)Kuanzia 10,000/= kutokana na mfuko uliochagua
MUDA WA UWEKEZAJIEndelevuMiaka kutokana na bondi husikaEndelevu au Miaka kutokana na mfuko husika
URAHISI WA KUIPATA PESA (LIQUIDITY)Utaweza kuuza pakiwa na wanunuaji sokoniUnaweza ukauza siku 2 za kazi baada ya manunuzi kukamilikaInaongoza kwa urahisi, kutokana na mfuko uliochagua 
HATARI YA KUPOTEZAKubwa ZaidiNdogo ZaidiWastani
UWEZEKAJI MCHANGANYIKO (DIVERSIFICATION)Uwekezaji ni hisa peke yakeUwekezaji ni bondi uliyonunuaUnaweza ukawa kwenye rasilimali tofauti kama hisa, bondi, na call accounts
GHARAMAMauzo na manunuzi huwa na makato ya kodi, ‘broker’/wakala, na taasisi za uwekezajiMakato ya kodi kwenye faida hayapo kwa bondi zaidi ya miaka miwiliMakato yanategemeana na mfuko
USIMAMIZI WA KITAALAMUWewe unafanya maamuzi ya uwekezajiWewe unafanya maamuzi ya uwekezajiWataalamu wa uwekezaji wanafanya maamuzi
USHAURI NA ELIMU KABLA YA KUWEKEZAInahitajika kwa kiwango kikubwaNi muhimuNi muhimu

Baada ya kujua haya, unaweza kuchagua ni uwekezaji upi unaanza nao, kama ni Bondi, Hisa, au Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji.

Na, 

unaweza ukapakua (download) tracker hapa chini kwa ajili ya urahisi wa kufuatilia uwekezaji wako kila mwezi:

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.

PS:

Malengo yako kwa kiasi kikubwa ndio yanakurahisishia safari yako ya uhuru wa kifedha.

Anza leo!

Kila la kheri.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz

2] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz

3] Bank of Tanzania, bot.go.tz

4] Watumishi Housing Investment, whi.go.tz

5] M-Wekeza, vodacom.co.tz6] Sanlam Pesa Money Market Fund, invest-tz.sanlameastafrica.com

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

Share your love
Grace Sambali
Grace Sambali
Articles: 55