Money Management – Gracing Money https://gracingmoney.com Begin. Grow. Sustain Sat, 14 Feb 2026 06:33:48 +0000 sw hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://gracingmoney.com/wp-content/uploads/2025/08/cropped-Gracing-Money-Icon-2-32x32.png Money Management – Gracing Money https://gracingmoney.com 32 32 Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust? https://gracingmoney.com/sw/umesikia-kuhusu-mifuko-sita-6-ya-uwekezaji-ya-itrust/ Sat, 17 Jan 2026 03:43:26 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2455 Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka

Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja…

Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo zaidi ya mifuko 18 hapa nchini kwetu.

Kama ndio mara ya kwanza kusikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji au haujajua namna ya kuchagua… 

mfuko wa uwekezaji unaoendana na malengo yako, naomba urejee kwenye ‘blog’ ambazo nimekwisha kuandika tayari.

Bila kupoteza muda, tuendelee.

Kama taasisi ya UTT (Unit Trust Tanzania) ilivyo na mifuko sita (6) ya Uwekezaji, 
Kampuni la iTrust pia lina mifuko sita (6) ya uwekezaji

…lenye madhumuni tofauti tofauti.


iTrust, ambayo kwa sasa bila ina leseni kama kampuni ya uwekezaji,  ilianzishwa Januari 2013…

lakini ilibadilishwa jina kuwa iTrust Finance Limited, Oktoba 2023.

Mifuko mitano (5) ya iTrust inayoonekana hapo chini, ilianzishwa Desemba 2024;

✔ iCash

✔ iGrowth

✔ iSave

✔ iIncome

✔ iImaan

Yote yenye kianzio cha 100,000/= isipokuwa iIncome (kianzio chake ni 10,000,000/=)

na unaweza ukatoa fedha ndani ya siku 3 za kazi baada ya fomu ya mauzo kupokelewa.

Mfuko wa mwisho, kwa sasa ni  iDollar

ulioanzishwa Agosti 2025. Kiasi chake cha kuanzia ni $1,000.

Mifuko ya iTrust

MfukoFaida YakeMfuko Unawekeza Pesa Kwenye…

iCash

Kukuza Mtaji na kuhifadhi fedha kwa muda mfupi
✔ Hatifungani za Serikali
✔ Hatifungani za Taasisi
✔ Rasilimali Nyingine

iGrowth

Kukuza Mtaji
✔ Hatifungani za Serikali
✔ Hisa
✔ Rasilimali Nyingine

iSave

Kukuza Mtaji na kuhifadhi pesa
✔ Hatifungani za Serikali

iIncome

Kutoa Mapato kila mwezi
✔ Hatifungani za Serikali

iImaan

Kukuza Mtaji
✔ Hatifungani (Sukuk)
✔ Amana za Kiislamu (Islamic Deposits)
✔ Hisa Halal zinazoendana na misingi ya Shariah

iDollar


Kulinda Mtaji na Kukuza Mtaji
✔ Dollar Financial Assets
✔ Hatifungani za Taasisi
✔ Amana za Muda Maalumu za nje ya nchi.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] iTrust Funds, https://www.itrust.co.tz/

2] UTT-AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
UTT ni nini? https://gracingmoney.com/sw/utt-ni-nini-2/ Fri, 16 Jan 2026 15:16:13 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2449 UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza.

Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini hujajua watu wanaongelea nini…

Au unajua kwamba ni UTT ina mifuko tofauti lakini hujajua hio mifuko ni kwa ajili gani.

Utakaposoma mpaka mwisho, utaweza kuelewa UTT ni nini hasa, na mifuko yake ina tofauti ipi,

tukianza na uwekezaji…

Kuwekeza ni kutumia fedha uliyokusanya au kuweka akiba ili kuzalisha fedha nyingine au faida.

Njia mojawapo ya kuwekeza ni kukusanya fedha pamoja na wawekezaji wengine halafu kugawana faida, hii ndo inaitwa Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji,


na UTT-AMIS (Unit Trust of Tanzania – Asset Management and Investor Services),

ni taasisi mama ya uwekezaji wa pamoja hapa kwetu Tanzania, ilioanzishwa mwaka 2003.

UTT inamilikiwa na serikali, chini ya Wizara ya Fedha.

UTT inafanyaje kazi?

Pesa za wawekezaji zinapokusanywa, zinawekezwa kwenye rasilimali nyingine za fedha kama Bondi, Hisa na Akaunti za Akiba za Muda Mfupi (Call Accounts).

 Uwekezaji wa fedha hizi unafanywa na wataalamu wa uwekezaji, na

..hii ni faida kubwa mojawapo ya kuwekeza kwenye mifuko ya pamoja.

Hatifungani (Bondi) mara nyingi huwa na kianzio cha 1,000,000/= na unapowekeza katika Hisa, inahitaji wewe mwenyewe kufuatilia.

Sio kila mtu anaweza kuwa na 1,000,000/= ya kuwekeza na sio kila mtu ana muda na utaalamu wa kufuatilia hisa,…

kwahio mifuko ya uwekezaji unasaidia watu wa hali zote kuweza kuwekeza.

Mifuko ya UTT inakuahidi ongezeko la pesa yako kwa angalau asilimia 12% kwa mwaka au angalau 1% kwa mwezi.

Mfano;

Unapowekeza au kuweka akiba ya 100,000/= leo, ndani ya mwaka hela inaweza ikakua mpaka 112,000/=

Lakini pia ni vizuri kujua,

Uwekezaji wowote lazima uje na hatari ya kupoteza (risk) ambayo inaweza ikawa kubwa au kidogo, kwasababu…

soko la fedha linaathiriwa na maendeleo ya uchumi nchini na duniani.

Mifuko ya UTT

UTT ina mifuko 6;

✔ Mfuko wa Watoto

✔ Mfuko wa Ukwasi

✔ Mfuko wa Wekeza Maisha 

✔ Mfuko wa Jikimu

✔ Mfuko wa Bond

✔ Mfumo wa Umoja

MfukoFaida YakeUnaweza Kutoa Fedha…Kianzio (Shilingi)
Watoto
Kukuza MtajiMpaka mtoto afike umri wa miaka 1210,000/=
UkwasiKukuza MtajiNdani ya siku 3 za kazi100,000/=
Wekeza MaishaKukuza MtajiBaada ya miaka mitano (5)8,340/= kwa mwezi, au
1,000,000/=
Jikimu
Kutoa GawioNdani ya siku 10 za kazi5,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
1,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwaka
2,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila robo mwaka
Bond
Kutoa GawioBaada ya miezi 3-650,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
5,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila baada ya miezi 6
10,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwezi
Umoja
Kukuza MtajiNdani ya siku 10 za kazi10,000/=

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz

2] UTT-AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
VITABU VITANO Vinavyoweza Kubadilisha Mtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO https://gracingmoney.com/sw/vitabu-vitano-vinavyoweza-kubadilishamtazamo-wako-kuhusu-pesa-yako/ Thu, 16 Oct 2025 16:52:42 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2227 Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako.

1. The Richest Man in Babylon / Tajiri wa Babeli

2. Rich Dad, Poor Dad / Baba Tajiri, Baba Maskini

3. The Psychology of Money

4. Maamuzi Juu ya Fedha Inayopita Mkononi Mwako Yaweza Kukufanya Uwe Tajiri au Maskini

5. Kustaafu

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Mbinu 7 ULIZOWAHI KUSIKIA Kuhusu Bajeti, Akiba, na Matumizi Hata Ukiwa na KIPATO KIDOGO https://gracingmoney.com/sw/mbinu-7-ulizowahi-kusikia-kuhusu-bajeti-akiba-na-matumizi-hata-ukiwa-na-kipato-kidogo/ Tue, 14 Oct 2025 08:45:38 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2053 Jifunze jinsi ya kuweka bajeti, kuepuka madeni, kuweka akiba, na kufuatilia matumizi hata ukiwa na kipato kidogo.

Kukosa nidhamu ya fedha haihusiani na ukubwa wa kipato. 

Changamoto kama kutokuwa na bajeti, kutoweka akiba, kutokumudu matumizi, hata kusongwa na madeni zinawakuta…

…wenye vipato vikubwa, wastani na vipato vidogo.

Unadhani ni kwanini?

Ni kwasababu, nidhamu ya fedha ni tabia. Na wewe ndiye unayeijenga tabia, kama utaridhia.

Ripoti ya Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Huduma za Kifedha nchini, FinScope Tanzania ya 2023, imeonyesha kwamba…

asilimia 66% ya watanzania wanapata changamoto kumudu gharama za kawaida za maisha.

Lakini pia, 


akiba ni kipaumbele baada ya mapato kwa watu asilimia 4% tu huku matumizi

(ukitoa chakula na mavazi) kuzidi kwa asilimia 77%.

Sasa, bila kupoteza muda, tukianza na mbinu za…

Kuwa na bajeti,

1. Ujue kutofautisha kati ya matumizi ya lazima ‘needs’ na yasiyo ya ulazima ‘wants’

Mara nyingi matumizi yasiyo na ulazima yana gharama zaidi kuliko matumizi ya msingi, na

…utapata msukumo zaidi kutumia pesa kwenye ‘wants’ kuliko kwenye ‘needs’.


Anza na matumizi yako ya msingi kama chakula, usafiri, na malazi.

2. Fuatilia matumizi yako yakoje, kila shilingi, angalau mara 1 kwa wiki.

Bajeti ya namna hii inaitwa ‘Zero-Based Budgeting’.

Ukifuatilia matumizi yako kwa angalau mwezi mmoja, utajua kirahisi udhaifu wako uko wapi.

Mfano;

Kama kipato chako ni 600,000/= kwa mwezi, baada ya mwezi kuisha utajua wapi unatumia hela zaidi,

…wapi wa kupunguza, wapi pa kuboresha au kurekebisha. Namba zitakupa majibu.

3. Weka akiba KABLA ya kufanya matumizi na sio kuweka akiba kwenye pesa iliyobaki.

Kwenye kuweka akiba,

Mfano;

Kama kipato chako ni 600,000/= kwa mwezi, tenga pembeni angalau asilimia 10% yani 60,000/= ndipo uanze kuipangia 540,000/=.

Itakua ngumu kwako kuweka akiba toshelevu ukishaanza kuitumia pesa mara tu unapoipokea.

4. Epuka kutumia pesa ili kuonekana na watu wengine au kwasababu ya matumizi unayoyaona kwa watu wengine.

Katika kumudu matumizi,

Kama wenzako wanaenda maeneo ya starehe ambayo huwezi kumudu kwa muda huo, usione aibu kulikubali hilo…

kwasababu hio ndio ‘urefu wa kamba yako kwa sasa’.

Wengine wakitoa michango ya sherehe ya 50,000/=, haina ubaya wowote kama wewe ukatoa unachokimudu.


Utakapotumia ili kuonekana, utapata stress ya pesa na watu wala hawatakuona.

5. Usitumie zaidi ya asilimia 30% ya kipato chako kwa ajili ya malazi ‘housing’

Jumla ya gharama za malazi kama kodi, umeme, maji, usafi na ulinzi zikiwa juu kulingana na kipato chako,

…utahangaika na matumizi mengine.

Kwa mfano;

Kama ni 600,000/= unaipata, halafu ukatumia zaidi ya 180,000/= kwa ajili ya nyumba kwa mwezi, inaweza ikawa ngumu…

kukitunaisha hicho kipato na mwezi unaofuata.

6. Usiache kutafuta fursa za kuongeza kipato na kuwa na malengo ya kifedha.

Kwa maana nyingine, usijikatie tamaa na ukaukubali umaskini. Uchukie umaskini.

Kuonewa huruma na kulalamika hakujawahi kumkomboa mtu, zaidi sana unaweza ukapata magonjwa kwasababu ya msongo wa mawazo.

Ni watu wengi wamezaliwa katika hali duni lakini hawajafa katika hali duni. Jione kama mmoja wao.

Kuna quote nzuri sana inasema,

You are born looking like your parents, You die looking like your decisions

Inamaanisha, unapozaliwa unafanana na wazazi wako ila unapokufa unafanana na maamuzi yako.

Kwahio, usikate tamaa mpaka unapotimiza unachokitamani.

Hakuna mtu wa kukufanyia hilo isipokuwa wewe.

7. Epuka madeni kwa kupunguza matumizi yasiyo ya msingi na kuweka akiba itakayoweza kukusaidia changamoto za ghafla zinapotokea.

Asilimia kubwa inayochukuliwa na watu ni kwa ajili ya matumizi binafsi, mbali na kuwekeza kuzalisha kwenye shughuli za uchumi.

Tunakopa kwa ajili ya,

✔ kuvaa vizuri, 

✔ kubadilisha furniture za ndani, 

✔ kutembelea gari kali, 

✔ kusafiri kwa ajili ya utalii, 

✔ kumudu gharama za misiba, 

✔ kuchangia sherehe,

✔ kulipa ada,

✔ kuhudumia ndugu na marafiki wasio na nidhamu ya pesa zao,

…lakini katika yote hapo juu, hakuna kinachozalisha pesa.

Zaidi ya kukuzalishia magonjwa na msongo wa mawazo.

Hakuna kibaya kati ya hivyo vyote…

lakini basi tafuta jinsi ya kuongeza kipato huku ukivifanya kwa kiasi.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS: 

Umezaliwa ukifanana na wazazi wako, lakini utakufa ukifanana na….(utamalizia) :)

Haujachelewa kuanza!

Kila la kheri.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

References:

1] FinScope Tanzania 2023 Key Findings Launch, 10th July 2023, Bank of Tanzania Auditorium

2] FinScope Tanzania 2023

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Ukweli Kuhusu MATUMIZI YAKO ya Fedha https://gracingmoney.com/sw/ukweli-kuhusu-matumizi-yako-ya-fedha-2/ Tue, 14 Oct 2025 08:16:07 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2047 Matumizi ya fedha yanaonyesha wewe ni mtu wa aina gani

Je, umezoea kuhudumia watu?

Au ni mwekezaji na unathamini akiba,

Unapenda starehe, sherehe, urembo, mapambo, vifaa vya kielekroniki…

Mkeka wako wa matumizi, utakusaidia kupata majibu.

Ripoti ya Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Huduma za Kifedha nchini, FinScope Tanzania ya 2023, imeonyesha kwamba…

matumizi (ukitoa chakula na mavazi) ni kipaumbele cha matumizi binafsi kwa asilimia 77%,

huku jambo kama akiba ni kipaumbele kwa asilimia 4% tu.

Matumizi yako yanaonyesha:

1. Vipaumbele Vyako

Matumizi yako ya awali na makubwa yatakuonyesha vitu gani ni muhimu kwako;

kula vizuri, kulipa madeni, kununua nguo, kuhudumia familia, kufurahisha marafiki,…

kutoka ‘out’, kuweka akiba ya matumizi ya msingi, kuendeleza biashara nk.

2. Nguvu Yako ya Kuweka Akiba na Kuwekeza

Ni asilimia ya mapato yako inaenda kwa ajili ya maisha yako ya baadae,

✔ Akiba ya Dharura

✔ Mfuko wa Kustaafu (hauhusiani na NSSF, PSSSF)

✔ Kujenga Nyumba

✔ Kuwekeza Kwenye Rasilimali Fedha kama Hisa, Bondi, nk.

Inawezekana matumizi yako yanaonyesha huweka akiba kabisa, unaweka akiba kidogo,…

au kipato chako kinapoongezeka, kipi kati ya matumizi na akiba kinaongezeka.

3. Kama Kipato Chako ni Pungufu, Kinatosha, au Haukimudu Vizuri

Kama kipato chako cha mwezi kinatumika kwa matumizi ya msingi tu na hakuna ziada, basi kipato ni pungufu kulingana na uhalisia wa maisha,

lakini pia inawezekana kipato chako kinatosha lakini hakikupi nafasi ya kutimiza malengo yako yote ya kifedha,…

au una kipato kikubwa lakini haukimudu vizuri.

Tathmini kipato chako kulingana na matumizi ya msingi, akiba, na malengo yako ya kifedha kujua kama ni vipi itakubidi kuongeza,

ili uishi maisha unayoyataka.

4. Nidhamu Yako ya Pesa

Je, unajali kuhusu akiba?

Unaweza ukajiambia hapana kama matumizi yanayokuja hayaendani na malengo yako?

Unaweza ukasema hapana kwa wale waliozoea kukuomba hela na unajua hawatarudisha?

Je, pesa yako unaielekeza kuendeleza biashara, uwekezaji, na malengo yako ya kifedha kama ulivyokusudia?

Uwezo wako wa kusema ndio au hapana ndipo nidhamu yako ilipo.

5. Maamuzi Gani Yanaharibu Bajeti Yako

Inaweza ikawa,

✔ Matumizi ya Dharura

✔ Mlolongo wa Madeni, au

✔ Kuhudumia familia na marafiki

Ukijua matumizi yako kwa angalau mwezi mmoja, utapata majibu yako kwa urahisi.

6. Ni Makosa Gani ya Kifedha Ambayo ni Tabia Kwako

Kama tulivyosema awali kwamba,

Matumizi yanatokana na tabia. Kama unaweka nia na mipango haitimiii, ni tabia gani inabidi kubadilisha kwa upande wako?

Mfano, kama yafuatayo ni kawaida;

✔ Matumizi ya Dharura ~ inabidi kujenga tabia ya kutanguliza akiba

✔ Mlolongo wa Madeni ~ kuachana na tabia ya kukopa

✔ Kuhudumia Familia na Marafiki ~ kufanya kwa kiasi na kusema hapana

Haijawahi kuwa rahisi kubadilisha tabia, hasa ya kwako mwenyewe. Hivyo kuwa na subira na tafuta mtu wa kukuwajibisha.

7. Hali Gani Zinakusukuma Kufanya Matumizi Ambayo Haukuyapanga

Inawezekana sio tabia, ni hali za mara moja moja.

Kama ni,

huzuni (utanunua unachokipenda upate furaha kwa huo muda mfupi),

furaha (utatumia hela kuongeza zaidi hali uliyonayo),

hasira (utanunua unachokipenda ushushe hio hasira kwa huo muda mfupi), au

aibu (hautaki kuaibika kwa mpenzi, marafiki au familia: hata kama huna).

Katika hali ya huzuni, hasira, na aibu, hela inatumika kama kipozeo cha unachokihisi ila haitatui sababu ya hali hiyo kuwepo.

Na pia, unaweza ukajifanyia tathmini ya uchumi binafsi kwa kujibu maswali machache, kama inavyoonekana hapa chini;

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na ujiunga na GM Free Community ya Whatsapp.

PS:

Ndani ya dakika 60, jengo lililojengwa kwa miaka mitatu (3) linaweza kuteketea kabisa kwa moto,

Na ndio ilivyo rahisi kuimaliza pesa uliotumia nguvu kuipata na kuikusanya kwa muda mrefu.

Kujua na kuzingatia namna unavyotumia pesa ni muhimu!

Kwako wewe na kwangu pia.

Kila la kheri.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] FinScope Tanzania 2023

]]>
Je, Uko Tayari KUUTAWALA UCHUMI WAKO Binafsi? Muongozo kwa Walio CHINI YA MIAKA 40! https://gracingmoney.com/sw/je-uko-tayari-kuutawala-uchumi-wako-binafsi-muongozo-kwa-walio-chini-ya-miaka-40-2/ Tue, 14 Oct 2025 07:30:50 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2023 Ni elimu muhimu ambayo hatukuwahi kupewa toka chekechea,

…au labda tungetakiwa kuipata katika ngazi ya kifamilia,

na ni nyumba chache sana za ibada zilizowapa waumini wake fursa ya kujifunza.

Halafu tukishamaliza madaraja yote ya elimu, tunarudi tena kwenye jambo hili hili,

Fedha, pesa, hela…

Tunarudi kwenye uchumi binafsi.

Maana uchumi wako halisi au uchumi unaotaka uonekana nao ndio utakusukuma kufanya maamuzi mengi,

yanayokuhusu wewe, watu wanaokutegemea, marafiki na aina ya maisha unayotaka kuishi.

Yaani kwa ufupi, jinsi utakavyohusiana na jamii nzima.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye uchumi wako, yote yako katika maamuzi yako, nayo ni;

✔ Kujijua Wewe,

✔ Kuijua Pesa Yako,

✔ Kujisimamia Wewe Mwenyewe, na

✔ Kuisimamia Pesa Yako.

Kitabu cha The Richest Man in Babylon cha George Clason, kwa kiswahili kimetafsiriwa kama Tajiri wa Babeli, kimetoa ufafanuzi mzuri wa…

misingi ya uchumi binafsi.

Mwandishi ameziita Tiba Saba (7) za Pochi Tupu.

Cha kwanza ni kuweka akiba, ya angalau asilimia 10 ya mapato yako.

Kwa lugha rahisi, usitumie kila kitu unachopata na usitumie zaidi ya unachokipata.

Kama unatumia zaidi, ina maana unakua umeshaingia kuignia kwenye madeni yasiyokurudishia faida.

Halafu dhibiti matumizi yako.

Jifunze kutofautisha kati ya mahitaji ya msingi na matumizi yasiyo ya msingi ili uweze kutumia chini ya unachopata.

Cha tatu, fanya pesa yako izae zaidi.

Wekeza akiba yako ili izalishe mapato ya ziada kupitia biashara au rasilimali zitakokuzalia faida.

Akiba isiyozalisha haitakufaidia kitu, zaidi sana utaendelea kuitumia hivyo itapungua.

Nne, linda pesa zako isipotee.

Epuka kuingia kwenye miradi yenye hatari/ risk kubwa ya kupoteza.  Fanya utafiti wako kabla ya kuwekeza au kujihusisha na biashara yoyote.

Kumbuka nguvu na muda uliyotumia kuipata pesa ni mkubwa kuliko muda unaoweza kuipoteza.

Tano, miliki nyumba/makazi yako.

Kuwa na makazi yako binafsi itakupa utulivu na huondoa gharama zisizo na lazima.

Lakini usisahau kwamba nyumba ni kwa ajili yako na familia, haikuzalishii chochote. Labda kama utafanya uwekezaji wa makazi ya kupangisha.

Sita, hakikisha una kipato cha baadaye.

Wekeza kwa ajili ya uzee na familia yako. Lenga usalama wa kifedha wa baadaye.

Mwisho ni kujiboreshea kielimu, kitaaluma, au kiuzoefu,

…katika ile kazi unayoifanya ili uongeze kipato chako kupitia ajira au biashara yako.

Kuelewa haya kunakupa mwanzo mzuri.

Na kama ungependa kujua zaidi kuhusu matumizi yako binafsi, unaweza ukasoma hapa.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na unaweza kujiunga na Whatsapp GM Free Community kwa kubonyeza button hapo chini.

PS:

Usisahau kwamba haya yote yanaanza na matumizi ya kile unachokipata. Malengo yako yatakueleza kama kipato chako kinatosha au la.

Na pia, haujachelewa kuanza!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] The Richest Man in Babylon, George S. Clason

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Hii ni AKIBA 1 Ambayo Hautakiwi Kuikosa, KWAKO na Kwenye Biashara YAKO! https://gracingmoney.com/sw/hii-ni-akiba-1-ambayo-hautakiwi-kuikosa-kwako-na-kwenye-biashara-yako/ Tue, 14 Oct 2025 07:23:53 +0000 https://fbp.rmj.mybluehost.me/website_74a27550/?p=1854 akiba, haiozi!

Je, umeshawahi kusikia kwamba ‘Siwezi kuweka akiba, hela yangu ni kidogo’?

Au labda unafikiri kwamba biashara inatakiwa kujiendesha yenyewe, hakuna haja ya kuwa na akiba.

Ingekuwa vizuri sana kama kabla ya changamoto yoyote kukutokea wewe au kwenye biashara yako, ingekupa taarifa…

Lakini, haitokei hivyo.

Hii akiba moja pia inaweza kukusaidia kupunguza au kuepuka kabisa ulazima wa kuingia kwenye madeni yenye riba kubwa,

…kwa sababu tu haujajiandaa.

Ripoti ya Uchumi ya mwezi Juni 2025 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kwamba mikopo binafsi ndio inayoongoza,

katika taasisi zote za fedha, katika mwezi Mei 2025, kwa asilimia 35.7% ikifuatiwa na biashara (trade) asilimia 13.7%…

Kama hali ni hii, unaweza ukaamua kuwa na akiba ambayo itafanya changamoto zikukute ukiwa umejiandaa,

…na amani ya moyo isitoweke ndani ya muda mfupi.

Na akiba hii ni Mfuko wa Dharura. Ni kiasi unachokusanya kwa ajili ya kukabiliana na yale usiyoyategemea.

Ukiwa na Mfuko wa Dharura:

✔ Kuisimamia Pesa Yako.

Unapata muda wa kutafuta kazi nyingine au kuanzisha biashara bila stress pale ambapo kipato kinaposhuka au kinapokata 

Inaondoa ulazima wa kuingia kwenye madeni, hasa yenye riba kubwa unapopata gharama za ghafla kwako na katika biashara yako

✔ Inakusaidia kuwa na amani unapokutana na changamoto kama ugonjwa au matengenezo ya gari

✔ Utaweza kuendeleza utaratibu wako wa kuweka akiba bila ulazima wa kukatisha

✔ Inakuwezesha kufanya maamuzi ndani ya muda mfupi kwenye dharura kama safari za lazima, misiba na changamoto za kifamilia…

…na kwenye biashara, pale panapokua na marekebisho ya nyenzo au vifaa vya kuendeshea biashara,

pia maamuzi ya haraka fursa zinapotokea.

✔ Inasaidia kutosumbua uwekezaji wako wa muda mrefu kwa sababu ya kutoa hela kwa ajili ya dharura

Utaweza kulipa bili za watoa huduma na kodi pale malipo ya huduma yako yanapochelewa

Kutopoteza heshima ya jina la biashara yako katika kutimiza ahadi ya huduma unayoitoa kwa wateja wako

✔ Kutunza heshima ya biashara yako kwa kuwalipa uliowaajiri kwa wakati, sawa sawa na mategemeo yao

Jinsi ya Kujua Kiasi cha Mfuko wa Dharura Kulingana na Matumizi Yako

Cha kwanza, inabidi kufahamu wastani wa matumizi yako kwa mwezi kisha uzidishe kwa miezi ambayo ungetaka kuilinda amani yako…

Miezi mitatu (3) mpaka 6.

Kama ni biashara, utatumia gharama kubwa zaidi uliotumia kuendesha biashara yako kuliko miezi mingine, kisha uzidishe mara 3 mpaka 6.

Unaweza ukajua hesabu yako sasahivi, kwa kutumia Emergency Fund Planner.

Kama ulikua haujawahi kuwa na malengo ya kifedha, umeshapata kiasi cha kuanzia kuweka akiba.

Unaweza pia ukatumia Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji kuweka akiba.

Pale utakapofanikiwa kukusanya kiasi kubwa, changamoto unayoweza ukaitegemea ni kutaka kutumia pesa kwa matumizi yasiyo ya lazima…

Ukipata msukumo huo, bila kusahau malengo yako, unaweza ukailinda pesa yako kwa kuiwekeza sehemu ambayo hautaweza kuitoa kirahisi sana


…kama Hisa na Bondi.

Pia, unaweza ukafahamu zaidi kuhusu Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji, Hisa na Bondi ndani ya dakika chache zijazo.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bonyeza hapo chini kujiunga na GM Free Community.

PS:

Kila 1,000,000/= ina shilingi 1,000/=, 2,000/=, na 5,000/= ndani yake. Usiidharau pesa ‘ndogo’.

Mfuko wa Dharura ni akiba ambayo hautakiwi kuikosa!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] Bank of Tanzania, Monthly Economic Review, June 2025.

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Hatua 7 Nyepesi za KUMALIZA NA KUYASAHAU MADENI Uliyonayo https://gracingmoney.com/sw/hatua-7-nyepesi-za-kumaliza-na-kuyasahau-madeni-uliyonayo/ Tue, 19 Aug 2025 16:18:09 +0000 https://fbp.rmj.mybluehost.me/website_74a27550/?p=1847 Tumia hatua hizi 7 rahisi kupunguza na kuondokana na madeni ili kuanza maisha ya uhuru wa kifedha.

Je, unawaza kukopa tena ili kupunguza madeni uliyonayo?

Au, unataka kumaliza madeni ila hujui uanze vipi…

Kama jibu lako ni ndio, barua hii ni kwa ajili yako.

Na watu wengi sana wako kwenye hali hii, si wewe peke yako!

Ripoti ya Uchumi ya mwezi Juni 2025 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kwamba mikopo binafsi ndio inayoongoza,

katika taasisi zote za fedha, katika mwezi Mei 2025, kwa asilimia 35.7%, ikifuatiwa na biashara (trade) asilimia 13.7%…

Hii inatuonyesha kwamba asilimia kubwa ya mikopo inayochukuliwa ni kwa ajili ya matumizi, kama…

✔ matibabu, 

✔ kugharamikia misiba, 

✔ kuchangia sherehe, 

✔ kupunguza madeni mengine, 

✔ kulipia shule/chuo,

✔ kununua magari,

✔ kujenga nyumba,

✔ kusafiri, 

✔ starehe nk.

na sio shughuli za kukuza uchumi.

Kama uko tayari, kuna hatua ambazo unaweza kuchukua ili kumaliza madeni yako;

1. Uikubali Hali Uliyonayo

Hatua ya kwanza ya matibabu ya ugonjwa ni kujua kwamba una changamoto fulani.

Je, kichwa kinauma, unashindwa kutembea, kuna uvimbe sehemu fulani?

Kama madeni yako ni kwa ajili ya matumizi, na unaishi maisha ya wasiwasi na aibu,…

usipoiona hio kwamba ni shida, watakachofanya watu wengine ni kukunyooshea vidole, hawatakutatulia.

Katika kuibali hali hii,

✔ andika madeni yako yote, 

✔ riba ya hayo madeni (kama unarudisha na faida), pamoja na 

✔ wote wanaokudai (kama ni watu au taasisi)

Halafu,

2. Urudi Mezani na Watu Wanaokudai

Kama kweli una nia wa kumaliza madeni yako, kwa ustaarabu ule ule uliiomba mkopo, rudi kwa watu wanaokudai,…

hii itakusaidia sana kuanza kujenga uaminifu uliokua umepotea.

Unaweza,

✔ ukaomba anayekudai akuongezee muda, 

✔ au akulegezee masharti

kwa ahadi kwamba utamrudishia kikamilifu kila anachokudai kadri ya unavyopata,

…na hio ahadi uitimize!

Kama aliyekukopesha hatakuelewa basi atakuambia anavyotaka kufidia mkopo wake kwa muda huo.

3. Utafute Mtu Atakayekuwajibisha

Anaweza akawa ni mwenza, rafiki, au mshauri wako wa fedha ambaye alikupa mbinu za kuyapunguza na kuyamaliza madeni.

Kama utapata sapoti ya mtu anayekujali na anayetaka ufanikiwe, utapata motisha zaidi.

Kumbuka kuna muda unaweza ukataka kukata tamaa au ukapata changamoto ukayumba kiuchumi,

…hii itakusaidia usirudi nyuma.

4. Upange Namna Utakavyolipa Madeni Uliyonayo

Hapa unakua umeshajua madeni gani unayapa kipaumbele, kama ni;

✔ madeni madogo kwanza (Debt Snowball), au 

✔ madeni yenye riba kubwa kwanza (Debt Avalanche), au 

✔ utajumuisha madeni yako yote halafu ukachukua mkopo mmoja wenye riba ya chini (Debt Consolidation)

Namna yoyote ile itakayokusaidia kulipa madeni yako kwa mpangilio.

Kumbuka maisha lazima yaendelee. Kuna mahitaji yako ya msingi, familia, na matamanio yako mengine…

kwahio, toa kipaumbele kwenye,

✔ matumizi ya msingi ya kila siku,

✔ asilimia ya mapato yako inayoenda kupunguza madeni, na

✔ kuanza kuweka akiba, hata kama ni kidogo, ikusaidie kwenye dharura yoyote

Kama ni kujinyima, itakua ni suala la muda.

Kama unaona kipato chako hakitoshi,

6. Ongeza Kipato

Tafuta namna ya kuongeza kipato, katika sehemu unayofanyia kazi au nje ya hapo.

Kupitia watu wanachokitaka au wanaokihitaji;

✔ ongeza wigo katika kile unachokifanya tayari; kama ni kutoa ushauri (consulting), kufanya kazi overtime (kama wanalipa masaa ya ziada)

✔ tumia ujuzi binafsi; kama kupika, ufundi, nk.

Namna yoyte itakayokupunguzia muda wa kuendelea kulipa deni lako.

Kumbuka kwamba kipato kutotosha mahitaji ndio ilikua sababu ya kuingia kwenye mlolongo wa madeni.

7. Anza Safari Mpya ya Uchumi Wako Binafsi

Kupitia akiba uliyoanza kuweka, usiache kuendelea kujifunza namna ya kumudu fedha yako.

Kama ni,

✔ kupunguza matumizi yasiyo ya msingi,

✔ kuongeza kipato

✔ kuweka akiba

✔ kuwekeza 

✔ kusaidia kwa kiasi, nk.

Baada ya haya yote, unaweza ukajua kiwango chako cha  madeni sasahivi kutumia hesabu ya ‘Debt-to-Income Ratio’ (DTI)

DTI inaonyesha uwiano kati ya malipo ya madeni yako kila mwezi na kipato chako.

Ukitumia hio calculator hapo chini…

Chini ya asilimia 36%: 


Inaonyesha kwamba unaweza kuyamudu madeni uliyonayo na unaweza kuweka akiba kwenye kiasi kinachobaki baada ya matumizi yako ya msingi.

Asilimia 36% mpaka 50%:

Kuna haja ya kuchukua hatua kupunguza madeni uliyonayo, kwasababu unaweza usiweze kumudu gharama za dharura, yaani…

matumizi muhimu ambayo haukuyategemea.

Na, zaidi ya 50%:


Unaweza ukakosa fedha ya kutosha
kwa ajili ya matumizi ya msingi, kuweka akiba na kumudu gharama za dharura.

Tumia hesabu hii pia, kabla ya hujachukua mkopo au kuongeza mkopo, ili ujue kama…

unaweza kulimudu hilo deni bila ‘stress’.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na jamii yetu ya GM Free Community.

PS:

Deni kwako lisiwe mzigo! 

Badala yake, tumia fedha unayopata kujenga vyanzo vingine vya pesa na sio kuziba unapoendelea kuvujisha.

Chukua hatua ili madeni umiza kwako yawe historia.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] Bank of Tanzania, Monthly Economic Review, June 2025.

2] Wells Fargo, Debt-to-Income Calculator.

3] The Richest Man in Babylon, George S. Clason

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>