Investments – Gracing Money https://gracingmoney.com Begin. Grow. Sustain Sat, 14 Feb 2026 07:02:09 +0000 sw hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://gracingmoney.com/wp-content/uploads/2025/08/cropped-Gracing-Money-Icon-2-32x32.png Investments – Gracing Money https://gracingmoney.com 32 32 Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust? https://gracingmoney.com/sw/umesikia-kuhusu-mifuko-sita-6-ya-uwekezaji-ya-itrust/ Sat, 17 Jan 2026 03:43:26 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2455 Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka

Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja…

Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo zaidi ya mifuko 18 hapa nchini kwetu.

Kama ndio mara ya kwanza kusikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji au haujajua namna ya kuchagua… 

mfuko wa uwekezaji unaoendana na malengo yako, naomba urejee kwenye ‘blog’ ambazo nimekwisha kuandika tayari.

Bila kupoteza muda, tuendelee.

Kama taasisi ya UTT (Unit Trust Tanzania) ilivyo na mifuko sita (6) ya Uwekezaji, 
Kampuni la iTrust pia lina mifuko sita (6) ya uwekezaji

…lenye madhumuni tofauti tofauti.


iTrust, ambayo kwa sasa bila ina leseni kama kampuni ya uwekezaji,  ilianzishwa Januari 2013…

lakini ilibadilishwa jina kuwa iTrust Finance Limited, Oktoba 2023.

Mifuko mitano (5) ya iTrust inayoonekana hapo chini, ilianzishwa Desemba 2024;

✔ iCash

✔ iGrowth

✔ iSave

✔ iIncome

✔ iImaan

Yote yenye kianzio cha 100,000/= isipokuwa iIncome (kianzio chake ni 10,000,000/=)

na unaweza ukatoa fedha ndani ya siku 3 za kazi baada ya fomu ya mauzo kupokelewa.

Mfuko wa mwisho, kwa sasa ni  iDollar

ulioanzishwa Agosti 2025. Kiasi chake cha kuanzia ni $1,000.

Mifuko ya iTrust

MfukoFaida YakeMfuko Unawekeza Pesa Kwenye…

iCash

Kukuza Mtaji na kuhifadhi fedha kwa muda mfupi
✔ Hatifungani za Serikali
✔ Hatifungani za Taasisi
✔ Rasilimali Nyingine

iGrowth

Kukuza Mtaji
✔ Hatifungani za Serikali
✔ Hisa
✔ Rasilimali Nyingine

iSave

Kukuza Mtaji na kuhifadhi pesa
✔ Hatifungani za Serikali

iIncome

Kutoa Mapato kila mwezi
✔ Hatifungani za Serikali

iImaan

Kukuza Mtaji
✔ Hatifungani (Sukuk)
✔ Amana za Kiislamu (Islamic Deposits)
✔ Hisa Halal zinazoendana na misingi ya Shariah

iDollar


Kulinda Mtaji na Kukuza Mtaji
✔ Dollar Financial Assets
✔ Hatifungani za Taasisi
✔ Amana za Muda Maalumu za nje ya nchi.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] iTrust Funds, https://www.itrust.co.tz/

2] UTT-AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
UTT ni nini? https://gracingmoney.com/sw/utt-ni-nini-2/ Fri, 16 Jan 2026 15:16:13 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2449 UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza.

Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini hujajua watu wanaongelea nini…

Au unajua kwamba ni UTT ina mifuko tofauti lakini hujajua hio mifuko ni kwa ajili gani.

Utakaposoma mpaka mwisho, utaweza kuelewa UTT ni nini hasa, na mifuko yake ina tofauti ipi,

tukianza na uwekezaji…

Kuwekeza ni kutumia fedha uliyokusanya au kuweka akiba ili kuzalisha fedha nyingine au faida.

Njia mojawapo ya kuwekeza ni kukusanya fedha pamoja na wawekezaji wengine halafu kugawana faida, hii ndo inaitwa Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji,


na UTT-AMIS (Unit Trust of Tanzania – Asset Management and Investor Services),

ni taasisi mama ya uwekezaji wa pamoja hapa kwetu Tanzania, ilioanzishwa mwaka 2003.

UTT inamilikiwa na serikali, chini ya Wizara ya Fedha.

UTT inafanyaje kazi?

Pesa za wawekezaji zinapokusanywa, zinawekezwa kwenye rasilimali nyingine za fedha kama Bondi, Hisa na Akaunti za Akiba za Muda Mfupi (Call Accounts).

 Uwekezaji wa fedha hizi unafanywa na wataalamu wa uwekezaji, na

..hii ni faida kubwa mojawapo ya kuwekeza kwenye mifuko ya pamoja.

Hatifungani (Bondi) mara nyingi huwa na kianzio cha 1,000,000/= na unapowekeza katika Hisa, inahitaji wewe mwenyewe kufuatilia.

Sio kila mtu anaweza kuwa na 1,000,000/= ya kuwekeza na sio kila mtu ana muda na utaalamu wa kufuatilia hisa,…

kwahio mifuko ya uwekezaji unasaidia watu wa hali zote kuweza kuwekeza.

Mifuko ya UTT inakuahidi ongezeko la pesa yako kwa angalau asilimia 12% kwa mwaka au angalau 1% kwa mwezi.

Mfano;

Unapowekeza au kuweka akiba ya 100,000/= leo, ndani ya mwaka hela inaweza ikakua mpaka 112,000/=

Lakini pia ni vizuri kujua,

Uwekezaji wowote lazima uje na hatari ya kupoteza (risk) ambayo inaweza ikawa kubwa au kidogo, kwasababu…

soko la fedha linaathiriwa na maendeleo ya uchumi nchini na duniani.

Mifuko ya UTT

UTT ina mifuko 6;

✔ Mfuko wa Watoto

✔ Mfuko wa Ukwasi

✔ Mfuko wa Wekeza Maisha 

✔ Mfuko wa Jikimu

✔ Mfuko wa Bond

✔ Mfumo wa Umoja

MfukoFaida YakeUnaweza Kutoa Fedha…Kianzio (Shilingi)
Watoto
Kukuza MtajiMpaka mtoto afike umri wa miaka 1210,000/=
UkwasiKukuza MtajiNdani ya siku 3 za kazi100,000/=
Wekeza MaishaKukuza MtajiBaada ya miaka mitano (5)8,340/= kwa mwezi, au
1,000,000/=
Jikimu
Kutoa GawioNdani ya siku 10 za kazi5,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
1,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwaka
2,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila robo mwaka
Bond
Kutoa GawioBaada ya miezi 3-650,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
5,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila baada ya miezi 6
10,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwezi
Umoja
Kukuza MtajiNdani ya siku 10 za kazi10,000/=

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz

2] UTT-AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME na Msimamo Wako wa Kiimani https://gracingmoney.com/sw/jinsi-ya-kuingia-kwenye-soko-la-fedha-bila-kwenda-kinyume-na-msimamo-wako-wa-kiimani-2/ Wed, 31 Dec 2025 05:27:31 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2437 Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani

Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya mtandao lakini…

Wewe ni muislamu na ungependa kuweka akiba na kuwekeza mahala ambapo panaendana na misingi yako ya imani.

Kuna wadau katika Soko la Fedha waliolifikiria hili, na walio kufikiria wewe.

Rasilimali za Fedha za Kiislamu (Islamic Financial Products) zinakua zimezingatia;

✔ Kanuni za Shariah katika uwekezaji na miamala inayofanyika,

Mgawanyo wa Hatari ya Kupoteza ‘Risk’ kati ya mkopaji

Na…

Upatikanaji wa Huduma za Kifedha kwa wale ambao kwao,  huduma za kibenki za kawaida haziendani na msingi wa kidini.

Rasilimali za Kuweka Akiba (Islamic Saving Products) kwa ajili yako ni;

Islamic Savings Account

Hii hazitofautiani na akaunti ya benki ya kawaida ila inakua na kanuni ya kukupatia sehemu ya faida na sio riba.

✔ Akaunti ya Mudarabah (Mudarabah Account)

Upande mmoja unatoa mtaji na upande mwengine (wewe) unatoa ujuzi halafu faida inagawanywa kwa makubaliano (predetermined ratios).

Na,

✔ Akaunti ya Wadi’ah (Wadi’ah Account)

Hii akaunti inakua inalinda mtaji wako kuliko kupata faida.

Rasilimali za Uwekezaji (Islamic Investment Products) kwa ajili yako ni;

Sukuk (Islamic Bonds)

Unapata mapato ya Hatifungani, yaani malipo ya kuponi yanatokana na faida inayopatikana na sio riba. 

Mfano mzuri ni Sukuk Bond ya KCB Bank na Sukuk Bond mbili (2) za Serikali ya Zanzibar (kwa Shilingi TZS na kwa Dollars $$)

Mudarabah (Profit Sharing)

Upande mmoja unatoa mtaji na upande mwengine (wewe) unatoa ujuzi halafu faida inagawanywa kwa makubaliano (predetermined ratios).

Musharakah (Joint Venture)

Mara nyingi hutumika katika miradi ya ujenzi.

Watu au taasisi tofauti zinachangia mtaji wa mradi halafu wanagawana faida au hasara kutokana na namna walivyochangia.

Murabaha (Cost-Plus Financing)

Benki inanunua rasilimali (an asset) kwa ajili yako na inauza kwa bei ya kupata faida. Halafu wewe, unalipa kwa awamu, pamoja na faida yake.

Ijara (Lease Financing)

Unakopeshwa rasilimali na utalipa kwa mfumo wa kodi. Halafu umiliki utakua ni wako pale muda wa hiyo kodi hio utakapoisha.

Je, rasilimali hizi ni kwa ajili ya waislamu peke yake?

Hapana…

Ila ni lazima uzingatie taratibu zote zinazohusiana na huduma hio. 

Tembelea tawi la benki unayoitumia ili kufahamu ni huduma gani za akiba na uwekezaji walizonazo, au…

Benki zinazo zingatia misingi ya Kiislamu kama hizo kama AMANA Bank na CRDB Al Baraka.

Je, ni mfuko wa pamoja wa uwekezaji unaotafuta kuanza nao?

Kuna Alpha Halal Fund ulioanzishwa na Alpha Capital Limited na,

mfuko wa iImaan ulioanzishwa na iTrust Finance Limited.

Kama umeshaanza uwekezaji au kuweka akiba kwa mfumo wa ‘liquid assets’…

Fuatilia Instagram kwa ajili ya free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS: 

Bado una nafasi ya kushiriki kwenye Soko la Fedha, kuweka akiba na kuwekeza kwa ujasiri.

Anza leo!

Kila la kheri.

Wako katika pesa,

Gracing Money!

References:

1] CRDB AlBarakah Banking,https://crdbbank.co.tz/en/for-you/al-barakah-banking

2] AMANA Bank | Islamic Bank in Tanzania, https://www.amanabank.co.tz/

3] Financial Educator Certification, Covenant Institute of Tanzania and Bank of Tanzania (BOT)

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? https://gracingmoney.com/sw/je-wewe-kuwekeza-kwenye-kampuni-la-nicol-utakua-ni-uamuzi-sahihi-2/ Fri, 12 Dec 2025 12:23:19 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2418

Mabadiliko ya bei za hisa ya NICOL

Oktoba 2020 (TZS)Septemba 2025 (TZS)Mabadiliko (%)
1651390742.42%

Ugawaji wa Gawio kwa miaka mitano iliyopita (TZS kwa kila hisa)

20202021202220232024
1037435370
20202021202220232024
2%5%6%5%6%

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Jinsi ya KUANZA Kuwekeza Kwenye Hatifungani (BONDS) https://gracingmoney.com/sw/jinsi-ya-kuanza-kuwekeza-kwenye-hatifungani-bonds/ Thu, 16 Oct 2025 16:19:49 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2207 Anza kuwekeza kwa usalama kupitia bondi. Mwongozo huu unakupa msingi mzuri kama mwekezaji unayeanza.

Hatua Muhimu 7 za Kuanza Kuwekeza Kwenye Bondi

  1. Kupata uelewa sahihi kuhusu Bondi

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Sababu 5 Nyepesi Kwa Nini Hauhitaji Kununua HISA YA SHILINGI 16,010/= Ili Kupata Faida Kubwa https://gracingmoney.com/sw/sababu-5-nyepesi-kwa-nini-hauhitaji-kununua-hisa-ya-shilingi-16010-ili-kupata-faida-kubwa/ Thu, 16 Oct 2025 15:29:07 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2130 Huna haja ya kununua hisa ya bei kubwa ili upate faida kubwa. Pitia sababu hizi 5 kwa manufaa yako.

1. Bei ya Hisa Haionyeshi Moja kwa Moja Faida ya Baadaye

2. Uchambuzi Utakaofanya Kabla ya Uwekezaji Utakupa Uhalisia

3. Bei ya Hisa Inaweza Kuwa Ghali Kuliko Thamani Halisi ya Kitabu

4. Kampuni Inaweza Isitoe Gawio Hata Kama Imepata Faida

5. Bei ya Hisa Inaweza Isibadilike kwa Muda Mrefu

Na kama ungependelea uwekezaji wa namna nyingine, unaweza kupitia Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji na Uwekezaji katika Hatifungani (Bonds).

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Maswali Matano (5) ya Kujiuliza UNAPOCHAGUA ‘BROKER’ wa Hisa na Bondi https://gracingmoney.com/sw/maswali-matano-5-ya-kujiuliza-unapochagua-broker-wa-hisa-na-bondi/ Thu, 16 Oct 2025 13:12:04 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2174 Usichague broker bila kujibu maswali haya matano (5) katika kuanza na kuendelea uwekezaji wako.

  1. Je, huyu broker ana Leseni?

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Soko Lenye Miamala Mpaka Shilingi 21,561,225,960/= KWA SIKU kwetu Tanzania https://gracingmoney.com/sw/soko-lenye-miamala-mpaka-shilingi-21561225960-kwa-siku-kwetu-tanzania/ Thu, 16 Oct 2025 12:37:35 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2161 Ijue nguvu ya soko la hisa la Tanzania na jinsi ya kunufaika na uwekezaji kwenye DSE.

Gracing Money!

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Kwa Wale WANAOTAKA KUWEKEZA KWENYE HISA lakini Wameshindwa Kuanza (Haya Mambo 5 Rahisi, Yataondoa Hofu Yako) https://gracingmoney.com/sw/kwa-wale-wanaotaka-kuwekeza-kwenye-hisa-lakini-wameshindwa-kuanza-haya-mambo-5-rahisi-yataondoa-hofu-yako/ Thu, 16 Oct 2025 11:52:16 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2149 Unatamani kuwekeza kwenye hisa za Tanzania lakini hauna uhakika namna ya kuanza? Soma mpaka mwisho ili uanze leo.

1. Maana ya Hisa

2. Hisa Zinakupaje Faida

3. Changamoto za Kuwekeza kwenye Hisa

4. Bei za Hisa na Jinsi ya Kuchagua

Na jambo letu la mwisho,

5. Unaanzaje Kuwekeza Katika Hisa

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>
Je, Unajua MFUKO GANI wa Uwekezaji Utaendana na Malengo Yako? (Ni Mambo Matano Rahisi ya Kufahamu!) https://gracingmoney.com/sw/je-unajua-mfuko-gani-wa-uwekezaji-utaendana-na-malengo-yako-ni-mambo-matano-rahisi-ya-kufahamu/ Thu, 16 Oct 2025 05:07:20 +0000 https://gracingmoney.com/?p=2121 Soma hii kabla haujachagua mfuko wa uwekezaji unaoendana na malengo yako ya kifedha.

Umesikia mifuko mingi ya pamoja ya uwekezaji na hujui uchague upi?

Kama jibu lako ni ndio, 

…mpaka mwisho wa ujumbe huu, utakuwa umeshapata majibu unayotafuta.

Lakini, anzia hapa kama haujafahamu kuhusu mifuko ya uwekezaji.

Kuna zaidi ya mifuko 15 ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini kwetu,…

baadhi ikiwa;

✔ Mfuko ya Umoja (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Watoto (UTT Amis) 

✔ Mfuko wa Bond (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Ukwasi (UTT Amis)

✔ Mfuko wa Faida

✔ M-Wekeza, na

✔ Mfuko wa Sanlam Pesa.

Kila mfuko una malengo yake na faida yake ya kuutofautisha, lakini swali ni je, malengo yako ni yapi?

Hili ndo swali moja rahisi ambalo kama utaweza kulijibu, maswali yako yote mengine utayajibu kwa haraka sana.

Tuanze na;

1. Aina ya Mapato ya Mfuko Husika

Faida mbili (2) kuu za mifuko ya pamoja ni Kukuza Mtaji na Kupata Gawio.

Kama haya ndo malengo makuu mawili, inamaana mfuko unaouchunguza ni kwa ajili ya sababu moja wapo;..

…kwamba lengo kubwa la mfuko huo ni kukuza mtaji au kutoa gawio.

Kutumia mifano saba ya mifuko kwenye ukurasa wa kwanza, Mifuko ya Watoto na Umoja inakuza mtaji na Mfuko wa Bond unatoa gawio,

…lakini pia,

2. Faida Maalum ya Mfuko Huo


Mfuko unaweza ukawa unakuza mtaji au unatoa gawio lakini unaweza ukawa na faida maalumu ambayo wewe hauhitaji.

Mfano;

Mfuko wa Watoto ni maalumu kwa watoto. Kwahio unaweza ukataka kukuza mtaji lakini sio kwa ajili ya mtoto.

Mfuko wa UTT wa Wekeza Maisha unakuza mtaji lakini huwezi ukatoa mpaka baada ya miaka mitano. Huu unawafaa zaidi wanaojiandaa kustaafu.

Mfuko wa Bond unatoa gawio kila mwezi na kila nusu mwaka, lakini wewe unaweza ukawa unahitaji gawio kila robo mwaka,

…kwahio itakubidi kuchagua mfuko mwengine.

Kingine ni,

3. Kianzio cha Kuwekeza Kwenye Mifuko

Ni muhimu kufahamu kiwango cha chini cha uwekezaji cha mfuko husika.

Kianzio cha mifuko mingi kama mifuko ya Umoja, Watoto, Faida, M-Wekeza ni 10,000/= na mingine 50,000/= (kama Mfuko wa Bond),…

100,000/= (for Liquid and iCash Funds), all depending on the type of income it provides, whether it is an income or capital growth.

4. Muda wa Uwekezaji

Unaweza ukachagua mfuko unaoendana na muda unaotaka kuwekeza, kama ni muda mfupi au muda mrefu.

Muda wa Kizuizi:

Mifuko kama Faida, Watoto na Wekeza Maisha inaweza ikachukua miezi mitatu mpaka miaka mitano ya kizuizi kwenye kutoa fedha.

Na kabla ya kuchagua mfuko ujue kama ni kweli hautahitaji kutoa pesa katika kipindi chote cha kizuizi.

Na la mwisho ni,

5. Urahisi wa Kutoa Fedha

Ukiachana na muda wa kizuizi,

Unatakiwa kujua kwamba unahitaji kutoa hela yako ndani ya muda mfupi,…

je, muda mfupi kwako ni siku ngapi?

Mfuko gani utakufaa utakapopata dharura?

Mifuko inatofautiana, kuanzia siku 3 hadi siku 10 za kazi (kama Mfuko wa Ukwasi, Umoja, na Timiza) au mfuko ambao unaweza kutoa hela hapo hapo

kama M-Wekeza (ya Vodacom na Sanlam Investments).

Kwa, M-Wekeza, unaweza ukatoa pesa kupitia M-Pesa.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kujiunga na WhatsApp GM Free Community.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz

2] Watumishi Housing Investment, whi.go.tz

3] M-Wekeza, vodacom.co.tz

4] Sanlam Pesa Money Market Fund, invest-tz.sanlameastafrica.com

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

]]>