UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza.

Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini hujajua watu wanaongelea nini…

Au unajua kwamba ni UTT ina mifuko tofauti lakini hujajua hio mifuko ni kwa ajili gani.

Utakaposoma mpaka mwisho, utaweza kuelewa UTT ni nini hasa, na mifuko yake ina tofauti ipi,

tukianza na uwekezaji…

Kuwekeza ni kutumia fedha uliyokusanya au kuweka akiba ili kuzalisha fedha nyingine au faida.

Njia mojawapo ya kuwekeza ni kukusanya fedha pamoja na wawekezaji wengine halafu kugawana faida, hii ndo inaitwa Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji,


na UTT-AMIS (Unit Trust of Tanzania – Asset Management and Investor Services),

ni taasisi mama ya uwekezaji wa pamoja hapa kwetu Tanzania, ilioanzishwa mwaka 2003.

UTT inamilikiwa na serikali, chini ya Wizara ya Fedha.

UTT inafanyaje kazi?

Pesa za wawekezaji zinapokusanywa, zinawekezwa kwenye rasilimali nyingine za fedha kama Bondi, Hisa na Akaunti za Akiba za Muda Mfupi (Call Accounts).

 Uwekezaji wa fedha hizi unafanywa na wataalamu wa uwekezaji, na

..hii ni faida kubwa mojawapo ya kuwekeza kwenye mifuko ya pamoja.

Hatifungani (Bondi) mara nyingi huwa na kianzio cha 1,000,000/= na unapowekeza katika Hisa, inahitaji wewe mwenyewe kufuatilia.

Sio kila mtu anaweza kuwa na 1,000,000/= ya kuwekeza na sio kila mtu ana muda na utaalamu wa kufuatilia hisa,…

kwahio mifuko ya uwekezaji unasaidia watu wa hali zote kuweza kuwekeza.

Mifuko ya UTT inakuahidi ongezeko la pesa yako kwa angalau asilimia 12% kwa mwaka au angalau 1% kwa mwezi.

Mfano;

Unapowekeza au kuweka akiba ya 100,000/= leo, ndani ya mwaka hela inaweza ikakua mpaka 112,000/=

Lakini pia ni vizuri kujua,

Uwekezaji wowote lazima uje na hatari ya kupoteza (risk) ambayo inaweza ikawa kubwa au kidogo, kwasababu…

soko la fedha linaathiriwa na maendeleo ya uchumi nchini na duniani.

Mifuko ya UTT

UTT ina mifuko 6;

✔ Mfuko wa Watoto

✔ Mfuko wa Ukwasi

✔ Mfuko wa Wekeza Maisha 

✔ Mfuko wa Jikimu

✔ Mfuko wa Bond

✔ Mfumo wa Umoja

MfukoFaida YakeUnaweza Kutoa Fedha…Kianzio (Shilingi)
Watoto
Kukuza MtajiMpaka mtoto afike umri wa miaka 1210,000/=
UkwasiKukuza MtajiNdani ya siku 3 za kazi100,000/=
Wekeza MaishaKukuza MtajiBaada ya miaka mitano (5)8,340/= kwa mwezi, au
1,000,000/=
Jikimu
Kutoa GawioNdani ya siku 10 za kazi5,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
1,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwaka
2,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila robo mwaka
Bond
Kutoa GawioBaada ya miezi 3-650,000/=Kwa ajili ya kukuza mtaji
5,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila baada ya miezi 6
10,000,000/=Kwa ajili ya gawio kila mwezi
Umoja
Kukuza MtajiNdani ya siku 10 za kazi10,000/=

Tumia tracker kama ilivyoonyeshwa hapa chini kwa urahisi wa kufuatilia uwekezaji wako kila mwezi.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.

PS:

Usisahau kwamba kila safari ndefu, ikiwemo uhuru wa kifedha, huanza na hatua moja, nayo ni hatua ya kwanza. 

Anza leo!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] UTT-AMIS, uttamis.co.tz

2] UTT-AMIS, Investment Assumption Calculator, Monthly Investment Plan

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

Share your love
Grace Sambali
Grace Sambali
Articles: 55

Leave a Reply

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *