
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi?
Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua na jibu refu.
Nikaona si vibaya nikushirikishe na sina mpango wa kukupotezea muda.
Kama wewe ni mtu unayetamani kuanza uwekezaji kwenye hisa au unataka uongeze kampuni jingine kwenye uwekezaji wako,
maelezo yafuatayo yatakusaidia kuamua.
Kama hufahamu…
NICOL (National Investments Company Limited) ni kampuni lililoanzishwa mwaka 1999 kusaidia watu kuwekeza kwa pamoja katika shughuli za kiuchumi.
NICOL wamewekeza kwenye sekta mbalimbali kama;
✔ Taasisi za Kifedha (kama benki; NMB na CRDB),
✔ Mawasiliano (Vodacom),
✔ Uzalishaji wa Viwanda (TBL),
✔ Ardhi na Majengo
✔ Rasilimali za Fedha kama hatifungani na amana za muda maalum, na
✔ Sekta nyinginezo…
Ripoti ya mwaka 2024, imeonyesha mgawanyo wa uwekezaji wa NICOL kama inavyoonekana hapo chini;

Mgawanyo wa uwekezaji ni 67% Hisa, 18% Hatifugani, 13% Ardhi na Majengo, 2% UTT, na
kwenye Hisa, kampuni ina takribani:
✔ NMB Bank ~ TZS Bilioni 150,
✔ DSE ~ TZS Bilioni 4,
✔ TBL ~ TZS Bilioni 1.1,
✔ CRDB ~ TZS Bilioni 1.4,
✔ Mjumuiko wa makampuni mengine kama TCC, VODACOM na TPCC, zaidi ya TZS Bilioni 1.07.
Okay,
trend muhimu wewe kufahamu ni kama;
Mabadiliko ya bei za hisa ya NICOL
| Oktoba 2020 (TZS) | Septemba 2025 (TZS) | Mabadiliko (%) |
| 165 | 1390 | 742.42% |
Ugawaji wa Gawio kwa miaka mitano iliyopita (TZS kwa kila hisa)
| 2020 | 2021 | 2022 | 2023 | 2024 |
| 10 | 37 | 43 | 53 | 70 |
Kampuni inavyotumia mtaji wa wamiliki ‘Shareholder’s Equity’ kutengeneza faida (ROE: Return on Equity)
| 2020 | 2021 | 2022 | 2023 | 2024 |
| 2% | 5% | 6% | 5% | 6% |
Katika blog ya Kuanza na Hisa, nilieleza kwamba katika kuchagua hisa ya kununua, hautaangalia bei ya hisa peke yake,
…bali pia utaangalia ubora wa kampuni na historia ya kampuni katika kuongeza faida kila mwaka, yaani
✔ Ukuaji wa Mapato (Revenue Growth)
✔ Ukuaji wa Faida Halisi (Net Income Growth)
✔ Faida kwa kila hisa (EPS: Earnings Per Share)
✔ Faida ya Mtaji (ROE: Return on Equity), nk.
Taarifa kama hizi za makampuni, sio NICOL peke yake, utazipata katika ripoti za kila mwaka (annual reports).
Kupata elimu sahihi ya hisa na kufanya tathmini rahisi kwa makampuni machache ambayo ungependa kuanza nayo,
…kutakupa urahisi wa kuamua kuwekeza kwenye kampuni la NICOL au kampuni lingine lolote kwenye DSE (Dar-es-Salaam Stock Exchange).
Ukitaka kujua zaidi kuhusu mahusiano kati ya bei ya hisa na faida utakayopata, unaweza ukasoma hapa.
Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na
na unaweza kununua nakala yako ya eBook ya Uwekezaji katika Hisa kwa shilingi 29,900/= tu!
Sambamba na kitabu hicho, utapata BURE kabisa;
✔ Stocks Investment Tracker (Excel/Google Sheets) kwa ajili ya kuweka kumbukumbuku ya manunuzi yako ya Hisa na Gawio utakalopata
✔ Quantitative Analysis Tool (Excel/Google Sheets) kufanya tathmini ya uwekezaji kutumia rekodi za kampuni zilizopita
✔ Dakika 30 za kujibu ya maswali yako pale unapoamua kuanza.
Bonasi zingekugharimu 122,750/=, lakini wewe utazipata zote bure.
Una guarantee kwamba,
… kama utashindwa kuanza uwekezaji ndani ya siku 7, basi utarudishiwa pesa yako yote na utakuwa umebaki na nakala yako ya eBook,
ambayo utaitumia kama utaamua kuanza uwekezaji kwa upya.
Bonasi ya Dakika 30 za BURE za kujibu maswali yako ya uwekezaji itakua ni siku 14 tu baada ya blog hii kutoka,
…hivyo usipange kukosa.

Bonyeza kitufe hapo chini 👇 kununua eBook yako.
Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na unaweza ukatuandikia kupitia Whatsapp.
PS:
Kiwango cha chini cha kununua hisa ya kampuni lolote ni hisa 10 tu! Hauhitaji pesa nyingi kuanza.
Cheering for you :),
Gracing Money!
References:
1] NICOL 2024 Annual Report, National Investments PLC
2] nicol.co.tz
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
