Anza kuwekeza kwa usalama kupitia bondi. Mwongozo huu unakupa msingi mzuri kama mwekezaji unayeanza.
Je, umesikia kuhusu bondi na haujaelewa ni kitu gani?, au
…umetamani kuanza lakini ungetaka kuelewa zaidi?
Kama jibu lako ni ndio, hii nakala ni kwa ajili yako.
Bondi ni uwekezaji ambao unaikopesha serikali au taasisi ili upate riba katika kipindi cha muda fulani.
Wewe unapokopesha, serikali au taasisi inapokea fedha hizo na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo au kufanya biashara ili kupata faida,
huku jukumu la kukulipa riba linabaki kama mlivyokubaliana.
Aina za hatifungani/bondi, ni kama;
✔ Bondi za Serikali,
✔ Bondi za Manispaa,
✔ Bondi za Makampuni, na
✔ Bondi za Kimataifa.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT: Bnk of Tanzania) inatoa ratiba ya bondi za serikali ya kila nusu mwaka ifikapo mwezi Juni na Desemba,
…kwenye tovuti ya BOT, na unaweza ukapata orodha ya bondi za taasisi ‘corporate bonds’ zilizo active kwenye tovuti ya DSE.
Ukiachana na kupata gawio la kuponi, ambalo mara nyingi huwa mara 2 kwa mwaka, hasa kwa bondi za serikali,
…faida nyingine za kuwekeza kwenye bondi ni kama;
✔ Kutumia bondi kupata mkopo
✔ Ni uwekezaji wenye risk ndogo ya kupoteza
✔ Unaweza ukatumia bondi kuweka akiba ya muda mrefu
Hatua Muhimu 7 za Kuanza Kuwekeza Kwenye Bondi
- Kupata uelewa sahihi kuhusu Bondi
…kupitia vitabu, au
semina na video zinazoandaliwa na wataalamu wa fedha za online au physical.
Itasaidia namna ya kuamua kiwango kizuri cha riba na bei za kununulia bondi kupata faida nzuri zaidi.
Kiwango cha riba huongezeka na muda wako wa uwekezaji.
2. Kuwa na pesa angalau kiwango cha chini cha kuanzia.
Bondi nyingi huanzia 500,000/= mpaka 1,000,000/= kama kiwango cha chini cha kuanzia.
Kama unataka ununue bondi lakini hauna kiasi hiki, unaweza ukawekeza kwenye Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji ambao,
…umewekeza kwenye bondi, pamoja na wawekezaji wengine.
3. Chagua broker au dealer utakayehusiana nae.
Hauwezi kununua au kuuza bondi kama mtu binafsi.
Broker ni wakala anayefanya biashara kwa niaba ya mteja (wewe au taasisi), na
Dealer ni wakala anayenunua na kuuza bondi kwa niaba yake mwenyewe, yani yeye anaweza akakuuzia bondi kwenye soko la upili,
…secondary market kama DSE.
Unaweza ukapata orodha ya brokers na dealers wenye leseni kwenye tovuti ya DSE.
4. Fungua Akaunti Yako
…ya CDS (Central Depository System) kupitia broker wako.
5. Utanunua Bondi
…kwa kupitia mnada wa kwanza kwenye primary market au,
bondi ambayo imeshawahi kununuliwa na ikauzwa tena kwenye soko la upili, secondary market kama DSE.
6. Utapata uthibitisho wa manunuzi
…inayojulikana kama proof of payment kutoka kwenye serikali au taasisi husika uliyonunua bondi yake.
7. Utafuatilia malipo ya kuponi zako
…kwenye tarehe zilizowekwa na aliyekuuzia bondi au kwa unaweza ukawa na tracker yako kufuatilia.
Unaweza kupakua (download) tracker ya kufuatilia uwekezaji wako wa liquid assets;

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Unaweza ukanunua bondi pia kupitia Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji ambao,
…umewekeza kwenye bondi, pamoja na wawekezaji wengine kama Mfuko wa Bondi ‘Bond Fund’ ya UTT AMIS.
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
References:
1] Bank of Tanzania, bot.go.tz
2] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
