Usichague broker bila kujibu maswali haya matano (5) katika kuanza na kuendelea uwekezaji wako.
Umeamua kuwekeza katika hisa na bondi lakini umejua ya kwamba huwezi ukazinunua mwenyewe,
…na kwamba utahitaji broker, kama dalali au wakala wa miamala yako.
Kama huyu ni wewe, basi ujumbe huu ndio wa kwako!
Soko la Hisa (DSE), ni soko kama Kariakoo, ila lemye bidhaa za pesa.
Brokers wanakutana sokoni kununua na kuuza hisa na bondi kupitia minada.
Soko liko ‘active’ Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni. Na soko linafungwa siku za sikukuu.
Kabla ya kuchagua broker ni muhimu kuamua ni bidhaa gani unataka kuuza na kununua lakini pia,…
bidhaa zote ambazo broker huyo, anauza na kununua kwa niaba ya wateja wake.
Kwa ufupi, uwe umeshajifunza unachohitaji kabla ya kutafuta broker.
Kumbuka broker,
✔ Anauza na kununua hisa na bondi kwa niaba yako
✔ Yeye hamiliki hisa wala bondi
✔ Analipwa hela ya udalali ‘commission’, na
✔ Habebi hatari / ‘risk’ iliyoko sokoni kwasababu yeye ni wakala tu
✔ Anakutumia taarifa za miamala yako ya hisa iliyokamilika
✔ Anakua na taarifa za akaunti yako ya hisa au bondi
Kuwa na majibu ya mambo haya matano yatakuokolea muda wako kwenye kufanya maamuzi;
- Je, huyu broker ana Leseni?
Broker awe anatambulika na mamlaka za uwekezaji, kama
DSE (Dar-es-Salaam Stock Exchange) na Mamlaka ya Masoko na Dhamana ‘CMSA’ (Capital Markets and Securities Authority)
Unaweza kupata orodha ya ‘brokers’ wenye leseni kwenye website ya DSE.
2. Ni broker mwenye Uzoefu?
broker mwenye biashara ya muda mrefu zaidi, amekuwepo nyakati tofauti za uchumi nchini na ana historia nzuri zaidi ya faida na hasara sokoni.
Lakini pia ameshakutana na hasara na changamoto nyingi zaidi, hivyo anaweza akakupa ushauri wa kina kwenye kufanya maamuzi.
3. Gharama za Huduma za kusimamia akaunti yangu zikoje?
Broker wanapata commission kutokana na miamala wanaoifanya.
Commission kwao ni ada na gharama kwa upande wako, kulingana na kiasi cha pesa unachonunulia hisa na bondi.
Unaweza ukatafuta kulinganisha gharama kati ya broker tofauti kwa kuuliza asilimia wanayokata kama ada ya udalali ‘Brokerage Commission’,
4. Huyu broker anatoa Huduma Nzuri kwa wateja?
…tafuta kujua kama wanahudumia changamoto za wateja kwa wepesi na uharaka.
Ukijiunga kwenye ma-group ya mtandaoni kama Whatsapp kuhusu uchumi binafsi, itakua rahisi wewe kupata majibu,
…kutoka kwa wawekezaji wengine.
Broker awe na namba zinazopatikana kwa urahisi wateja wanapohitaji msaada.
5. Ni broker anayefanya Utafiti wa Soko la Fedha?
broker mzuri hufanya utafiti na kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu hali ya soko kwa bidhaa zote anazofanyia udalali.
Ukianza na majina machache tu, unaweza kuangalia kwenye website zao lakini pia kurasa zao za mitandao ya jamii kama Instagram.
Unaweza kupakua (download) tracker ya kufuatilia uwekezaji wako wa liquid assets;

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Kiwango cha chini cha kununua ni hisa 10 tu! Hauhitaji mamilioni kuanza.
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
Marejeo:
1] Frequently Asked Questions About Dar-es-Salaam Stock Exchange Document
2] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
