Ijue nguvu ya soko la hisa la Tanzania na jinsi ya kunufaika na uwekezaji kwenye DSE.
Ijue nguvu ya soko la hisa la Tanzania na jinsi ya kunufaika na uwekezaji kwenye DSE.


Miamala ya Hisa,


Na miamala ya Bondi.
DSE lilianzishwa mwaka 1996, na kama tu ilivyo Kariakoo, Mbagala Sokoni…
DSE ni soko lenye bidhaa za pesa, kama Hisa na Bondi.
Soko liko ‘active’ Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni. Na soko linafungwa siku za sikukuu.
Cha muhimu kabla ya uwekezaji wowote ni kufahamu kile unachokwenda kuwekeza pesa zako.
Elimu sahihi ndio msingi wako.
Kwa Upande wa Bondi,
Kuna bondi za serikali ‘Treasury Bonds’ na za taasisi ‘Corporate Bonds’.
Bondi ‘active’ ni zile ambazo muda wake haujaiva bado, tarehe ya ‘bondi kumalizika ‘maturity’, haujafika.
Ingawa kiwango cha chini cha uwekezaji kinaweza kikawa kuanzia mpaka 500,000/= mpaka 1,000,000/=, sokoni bondi inauzwa…
kwa mafungu ya laki moja moja (100,000/=).
Wawekezaji wadogo wasioweza kuanza na kiasi hiki wanaweza kukusanya hela zao, kama ilivyo kwenye Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji
… na wakanunua bondi kupitia wakala, maarufu kama ‘broker’. Broker ananunua hisa na bondi kwa niaba yako (kama dalali),
kwasababu sokoni mwekezaji hanunui na kuuza bondi wala hisa kama mtu binafsi.
Kuchagua broker atakayekuwakilisha ni jukumu lako.
Kwenye Hisa,
Soko hili sasa liko mtandaoni ‘DSE Online Trading’ maarufu kama Hisa Kiganjani,…
unaweza ukapakua (download) app ya simu yenye jina hilo hilo, kisha ufuate maelekezo kuisajili na kuchagua broker.
Ukiwa sokoni, unaweza ukaona,
✔ makampuni yote na bei za hisa zake
✔ idadi ya hisa zinazouzwa kwa muda huo ‘Buy Stock’
✔ oda za kuuza na kununua ulizoweka sokoni ‘Buy Orders, Sell Orders’
✔ kiasi cha hisa na bondi ulizonazo (miamala iliyokamilika) ‘Holdings’
✔ makampuni ambayo yanauza hisa kwa mara ya kwanza ‘IPO – Initial Public Offering’
✔ taarifa za akaunti yako, akaunti za watoto chini yako, na taarifa za broker wako ‘Account Information’
Kikawaida, hisa na bondi zinanunuliwa kwa mnada. Kama minada ya kawaida tuliyoizoea,…
bidhaa inatangazwa halafu wananunuaji, wanatoa bei nzuri zaidi kuzidi wengine ili kununua.
Kutumia app yako ya Hisa Kiganjani kununua hisa, utafanya order ya kununua ‘buy order’,…
halafu utafanya malipo kwa kupitia control number na utasubiri mpaka siku 3 za kazi kujua kama,
order yako ya manunuzi imekubaliwa ‘fulfilled’ au
order yako ime-expire na itabidi kununua tena ‘repost order’.
Manunuzi yako yanapotimia, ‘broker’ wako atakutumia risiti/taarifa yako.
Kwa changamoto zozote za kiufundi unaweza ukawasiliana na broker wako au namba za DSE kupata msaada ndani ya muda ‘active’ wa soko.
Unaweza kupakua (download) tracker ya kufuatilia uwekezaji wako wa Hisa, pale unapoanza:

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Kiwango cha chini cha kununua ni hisa 10 tu! Hauhitaji mamilioni kuanza.
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
Marejeo:
1] Frequently Asked Questions About Dar-es-Salaam Stock Exchange Document
2] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
