Unatamani kuwekeza kwenye hisa za Tanzania lakini hauna uhakika namna ya kuanza? Soma mpaka mwisho ili uanze leo.
Inawezakana umetamani kuanza lakini hujajua namna…
Au umeshasikia lakini ungetamani kujua zaidi.
Endelea kusoma na utagundua si ngumu kama unavyodhani.
Kuna mtoto mmoja nchini Marekani, aliyeanza kuuza soda na magazeti akiwa na umri wa miaka 6,
na alinunua hisa za kwanza za kampuni la Citizen Service akiwa na miaka 11 tu.
Baada ya kupata faida kidogo, aliamua kuziuza na mara baada ya kuziuza, zilipanda bei kwa kasi.
Akawa amejifunza kwamba uvumilivu ni muhimu katika kuwekeza.
Alipokua kijana alichunguza kwa kina sana makampuni na thamani zake halisi ili aweze kununua hisa za kampuni bora lakini pia kwa bei nafuu.
Akaja akapata rafiki, kwa jina la Charlie, ambaye alimfundisha kutafuta biashara bora zaidi badala ya kutumia bei nafuu peke yake.
Kwa kuanza na pesa za familia yake katika uwekezaji, kijana huyu alinunua hisa za makampuni kama Coca-Cola, American Express, na Apple.
Yeye na Charlie, kupitia kampuni lao la Berkshire Hathaway, waliendelea kujikita kwenye biashara ambazo ni;
✔ rahisi kuelewa,
✔ zenye uongozi mzuri, na
✔ zenye uwezo wa kutoa faida ya kudumu.
Jina la mtu huyu ambaye ukiwa ni mwaka 2025, ana umri wa miaka 94 anaitwa Warren Buffet,
…na hisa moja, hisa ya daraja A, yaani Class A, ya kampuni yake ya uwekezaji, inauzwa zaidi ya dola 725,000 (takribani shilingi bilioni 2 za kitanzania).
Tukirudi kwenye mada yetu, mambo matano (5) muhimu na rahisi kuyajua ni…
1. Maana ya Hisa
Hisa ni umiliki wa sehemu ya kampuni au biashara. Kwa kiingereza inajulikana kama stock.
Hisa huuzwa kwa idadi na kwa bei ya kampuni husika yaani, stock price.
Kwahio, kama hisa moja ya kampuni X ni shilingi 1,000/= ina maana shilingi 10,000/= inakupa umiliki wa hisa 10 za kampuni X.
Unaweza ukafahamu zaidi kuhusu makampuni yaliyoko kwenye Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE, Dar-es-Salaam Stock Exchange), kupitia tovuti yao.
Mfano wa makampuni ya kitanzania ni Benki ya CRDB, Benki ya NMB, Tanzania Breweries (TBL), na Tanzania Portland Cement (Twiga Cement -TPCC).
2. Hisa Zinakupaje Faida
Kutokana na ushindani katika soko la Hisa, bei za hisa hupanda na kushuka (demand and supply).
Watu na taasisi huuza hisa zinapopanda bei kuliko ile walionunulia (capital gain). Hii ndo faida ya kwanza.
Mfano;
kama leo unanunua hisa moja ya kampuni X kwa shilingi 1,000/= na baada ya miezi miwili, bei ya hisa imekuwa 1,400/=, una faida ya 400/= kwa kila unayomiliki.
Mwezi Julai, 2024, bei ya hisa moja ya benki ya CRDB ilikua shilingi 600/=, lakini kufikia Julai 2025, bei ya hisa imekua shilingi 840/=.
Uwekezaji wa hisa unaweza kukuzalia matunda ya kudumu unapotamani kufanya kwa muda mrefu zaidi, long-term mindset.
Faida ya pili ni kupata gawio (dividend income), kwa kawaida mara 1 kwa mwaka.
Kulingana na faida waliopata kampuni husika katika mwaka wao wa fedha, baadhi ya makampuni hugawanya faida hiyo kwa wawekezaji.
Utakapopata gawio, utaamua kuiwekeza tena au kuitumia kivingine.
3. Changamoto za Kuwekeza kwenye Hisa
Uwekezaji makini (smart investing) ni ule ambayo utaelewa hatari ya kupoteza pia ili ufanye maamuzi kwako.
Kuwekeza katika Hisa una hatari zaidi ya kupoteza ukilinganisha na Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji na Hatifungani (Bonds).
Kutokua na ufahamu sahihi kabla ya kuwekeza ni changamoto inayowakumba wawekezaji wengi. Fahamu ya kwamba;
✔ Wewe mwenyewe, unapaswa kuielewa hisa, makampuni tofauti, mabadiliko ya bei, namna hisa inavyofanya kazi na jinsi ya kuchagua.
Unaweza ukatafuta mwalimu au mtaalamu wa fedha kukurahishia hili zoezi. Katika mifuko ya pamoja, wataalamu hufanya hivi kwa niaba yako.
✔ Inakubidi kufuatilia maendeleo ya kampuni unayowekeza.
Kufahamu taarifa yatakupa kuamua kuendelea kuwekeza, kuuza au kupunguza uwekezaji wako.
Lakini kuwa kwenye jamii za mtandaoni (kama Whatsapp Communities) za mambo ya fedha, inaweza kukurahishia kujua yanayotokea sokoni.
✔ Uwekezaji wako uendane na uthubutu wako wa kupoteza (Risk Appetite)
Hisa inaweza ikaleta faida kubwa sana ya kuongezeka mtaji ‘capital gain’ lakini pale ambapo kampuni halitafanya vizuri au likafa,
…hisa zinaweza zikashuka sana bei au ukashindwa kabisa kuziuza.
4. Bei za Hisa na Jinsi ya Kuchagua
Kama tulivyoona kwenye maana ya hisa,
…hisa zinatofautiana bei kulingana na kampuni wenyewe walivopata thamani yao ya kitabu.
Mnamo tarehe 4 Julai 2025, makampuni yaliyopo DSE ambayo yaliuza na kununua hisa kwa siku hio,
bei zilianzia shilingi 145/= (DCB: Commercial Bank) mpaka shilingi 16,010/= (TCC: Tanzania Cigarette Company – Sigara) kwa hisa moja.
Kama tulivyoona kwenye stori yetu mwanzoni ya Warren na Charlie, faida haitokani na bei ya hisa kuwa nafuu peke yake bali pia katika,
…ubora wa kampuni na historia yake ya kuongeza faida kila mwaka (ROE: Return on Equity).
Na jambo letu la mwisho,
5. Unaanzaje Kuwekeza Katika Hisa
Baada ya kupata elimu sahihi ya hisa na kuchagua kampuni la kuwekeza,
utachagua broker au wakala wa kukuuzia na kukunulia hisa.
Halafu, utaweka order kupitia app ya Hisa Kiganjani, au tovuti/website ya DSE, au kupitia broker wako kulingana na makubaliano yenu.
Utakapoweka order ya kununua ‘buy order’, utafanya malipo kwa kupitia control number na utasubiri mpaka siku 3 za kazi,
kujua kama order yako ya manunuzi imekubaliwa ‘fulfilled’ au order yako ime-expire na itabidi kununua tena ‘repost order’.
Manunuzi yako yanapotimia, ‘broker’ wako atakutumia risiti/taarifa yako.
Hapa chini, unaweza kupakua (download) tracker ya kufuatilia uwekezaji wako wa Hisa, pale utakapoamua kuanza:

Ukitaka kujua kuhusu mahusiano kati ya bei ya hisa na faida utakayopata, unaweza ukasoma hapa.
Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi WhatsApp.
PS:
Kiwango cha chini cha kununua ni hisa 10 tu! Hauhitaji mamilioni kuanza.
Kila la kheri.
Wako katika pesa,
Gracing Money!
Marejeo:
1] Dar-es-Salaam Stock Exchange Market Report, Friday, 4th July 2025.
2] Dar-es-Salaam Stock Exchange, dse.co.tz
Follow us on Socials

Read More Blog Posts
Umesikia Kuhusu Mifuko Sita (6) ya Uwekezaji ya iTrust?
Mifuko ya Uwekezaji ni mingi…na itazidi kuongezeka Je, umesikia kuhusu Mifuko ya Uwekezaji ya Pamoja… Imeongezeka na itaendelea kuongezeka. Kwa sasa ipo…
UTT ni nini?
UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…
Jinsi ya Kuingia Kwenye Soko la Fedha BILA KWENDA KINYUME
Mwongozo wa Muislamu Kushiriki Soko la Fedha kwa Njia Halali na ya Kiimani Umesikia watu wanaongea kuhusu uwekezaji, kila kona ya…
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi
Je, Wewe Kuwekeza Kwenye Kampuni la NICOL Utakua ni Uamuzi Sahihi? Kwenye picha hapo juu ni swali zuri nimeshawahi kuulizwa, na lilikua…
Jinsi ya Kuendesha Biashara Yako BILA KUPOTEZA UHURU Wako wa
Soma mpaka mwisho kama, una biashara ya kutoa huduma (service based business) au kuuza bidhaa (brick-and-mortar business), lakini unakabiliana na changamoto hizi; ✔…
VITABU VITANO Vinavyoweza KubadilishaMtazamo WAKO Kuhusu Pesa YAKO
Unataka kubadilisha mtazamo wa uchumi wako? Vitabu hivi vitano (5) vinaweza kubadilisha unavyofikiri kuhusu kipato, akiba na kukuza pesa yako. 6…
