Je, Uko Tayari KUUTAWALA UCHUMI WAKO Binafsi? Muongozo kwa Walio CHINI YA MIAKA 40!

Ni elimu muhimu ambayo hatukuwahi kupewa toka chekechea,

…au labda tungetakiwa kuipata katika ngazi ya kifamilia,

na ni nyumba chache sana za ibada zilizowapa waumini wake fursa ya kujifunza.

Halafu tukishamaliza madaraja yote ya elimu, tunarudi tena kwenye jambo hili hili,

Fedha, pesa, hela…

Tunarudi kwenye uchumi binafsi.

Maana uchumi wako halisi au uchumi unaotaka uonekana nao ndio utakusukuma kufanya maamuzi mengi,

yanayokuhusu wewe, watu wanaokutegemea, marafiki na aina ya maisha unayotaka kuishi.

Yaani kwa ufupi, jinsi utakavyohusiana na jamii nzima.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye uchumi wako, yote yako katika maamuzi yako, nayo ni;

✔ Kujijua Wewe,

✔ Kuijua Pesa Yako,

✔ Kujisimamia Wewe Mwenyewe, na

✔ Kuisimamia Pesa Yako.

Kitabu cha The Richest Man in Babylon cha George Clason, kwa kiswahili kimetafsiriwa kama Tajiri wa Babeli, kimetoa ufafanuzi mzuri wa…

misingi ya uchumi binafsi.

Mwandishi ameziita Tiba Saba (7) za Pochi Tupu.

Cha kwanza ni kuweka akiba, ya angalau asilimia 10 ya mapato yako.

Kwa lugha rahisi, usitumie kila kitu unachopata na usitumie zaidi ya unachokipata.

Kama unatumia zaidi, ina maana unakua umeshaingia kuignia kwenye madeni yasiyokurudishia faida.

Halafu dhibiti matumizi yako.

Jifunze kutofautisha kati ya mahitaji ya msingi na matumizi yasiyo ya msingi ili uweze kutumia chini ya unachopata.

Cha tatu, fanya pesa yako izae zaidi.

Wekeza akiba yako ili izalishe mapato ya ziada kupitia biashara au rasilimali zitakokuzalia faida.

Akiba isiyozalisha haitakufaidia kitu, zaidi sana utaendelea kuitumia hivyo itapungua.

Nne, linda pesa zako isipotee.

Epuka kuingia kwenye miradi yenye hatari/ risk kubwa ya kupoteza.  Fanya utafiti wako kabla ya kuwekeza au kujihusisha na biashara yoyote.

Kumbuka nguvu na muda uliyotumia kuipata pesa ni mkubwa kuliko muda unaoweza kuipoteza.

Tano, miliki nyumba/makazi yako.

Kuwa na makazi yako binafsi itakupa utulivu na huondoa gharama zisizo na lazima.

Lakini usisahau kwamba nyumba ni kwa ajili yako na familia, haikuzalishii chochote. Labda kama utafanya uwekezaji wa makazi ya kupangisha.

Sita, hakikisha una kipato cha baadaye.

Wekeza kwa ajili ya uzee na familia yako. Lenga usalama wa kifedha wa baadaye.

Mwisho ni kujiboreshea kielimu, kitaaluma, au kiuzoefu,

…katika ile kazi unayoifanya ili uongeze kipato chako kupitia ajira au biashara yako.

Kuelewa haya kunakupa mwanzo mzuri.

Na kama ungependa kujua zaidi kuhusu matumizi yako binafsi, unaweza ukasoma hapa.

Pia, jifanyie tathmini ya uchumi binafsi kwa kujibu maswali machache, kama inavyoonekana hapa chini;

Utatumiwa majibu yako kwenye email ili ugundue wapi pa kuanza kuboresha.

Usiache kufuatilia ukurasa wa Instagram kupata free content, na unaweza kuwasiliana nasi kwa Whatsapp na tutakurudia kwa wakati.

PS:

Usisahau kwamba haya yote yanaanza na matumizi ya kile unachokipata. Malengo yako yatakueleza kama kipato chako kinatosha au la.

Na pia, haujachelewa kuanza!

Wako katika pesa,

Gracing Money!

Marejeo:

1] The Richest Man in Babylon, George S. Clason

Follow us on Socials

Read More Blog Posts

UTT ni nini?

UTT ni nini?

UTT ni njia rahisi ya kuwekeza kwa watanzania. Elewa inavyofanya kazi na jinsi ya kuanza kuwekeza. Inawezekana umesikia kuhusu UTT lakini…

Share your love
Grace Sambali
Grace Sambali
Articles: 55